MWAKA MMOJA LEO BILA DK.SENGONDO MVUNGI
Na Happiness Katabazi
LEO Novemba 12 Mwaka 2014, Mhasisi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB),
Dk.Sengondo Mvungi Ametimiza Mwaka mmoja tangu alipofariki Dunia .
Dk.Mvungi alifariki dunia tarehe kama ya Leo Hospitali Milpark nchini
Afrika Kusini ambako alikuwa amelazwa kwaajili ya kupatiwa matibabu
baada ya usiku wa kuamkia Novemba 3 Mwaka 2013 kuvamiwa na wahalifu na
kujeruhiwa vibaya maeneo Mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kichwai na
hivyo kumsababishia majeraha makubwa na kupoteza fahamu tangu siku hiyo
hadi anafariki Dunia.
Kwangu Mimi binafsi nitaendelea kumkumbuka Dk.Mvungi Kwani nilimheshimu
sana na alikuwa ni mtu wangu wa karibu na ndiyo uwa nikimkubuka Mzee
wangu Huyo ambaye alikuwa akipenda kunitia Mimi ni Mkewe 'First Lady'
na Mimi Namuita yeye ni ' Rais Mdhulumiwa' uwa nakosa raha ila sina la
kufanya zaidi kuzingatia Yale aliyokuwa akinihusia ni yafanye kwa
uzalendo wa taifa langu na Maisha yangu binafsi.
Mbali ya Dk.Mvungi Kuuwawa akiwa na wadhifa wa Mjumbe wa Tume ya
Madiliko ya Katiba , pia Mvungi alikuwa ni miongoni wa wahasisi wa Chuo
Kikuu Cha Bagamoyo (UB) na ndiye aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Bagamoyo anayeshughulikia Taaluma.
Dk.Mvungi Leo ukiwa unatimiza Mwaka mmoja tangu ufariki, napenda
kukwambia kuwa UB, imekuwa sasa wanafunzi ni wengi wanazidi kujiunga
Katika chuo hicho kadri siku zinavyozidi kwenda Taasisi ya Vyuo
Kikuu(TCU)
Inakipatia chuo idadi ya wanafunzi.
UB ilianzishwa rasmi Mwaka 2011. Ushahidi wa UB inakuwa ni kwa hatua ya
TCU kuzidi kuleta idadi kubwa ya wanafunzi waje kusoma UB kozi
mbalimbali ni huu.
Katika mwaka wa kwanza wa masomo wa chuo hicho kilipoanzishwa
ulitambulika kuwa ni mwaka wa 2011/2012 chuo kilianza kikiwa na jumlanya
wanafunzi 64 tu.
Mwaka wa masomo wa 2012/2013 TCU ilipeleka jumla ya wanafunzi 154.
Mwaka 2013/2014 wanafunzi 234. Na mwaka mpya wa masomo ulioanza Novemba
tatu mwaka 2014 yaani Mwaka wa masomo wa 2014/2015 jumla ya wanafunzi
254 la Katiba.
Licha ya Mahalu kuwa mjumbe wa bunge hilo pia ndiye aliyekuwa Mwenyekiti
wa Kamati ya kutunga Kanuni zilizoliongoza Bunge kufanyakazi zake na
pia Mahalu alikuwa ni mjumbe wa Kamati ya kuandika Katiba
iliyopendekezwa na Bunge Hilo kuanzia Februali 18 hadi Oktoba 4 Mwaka
2014. usajili na wameanza masomo na kuna wanafunzi wengine bado
wanaendelea kufanya usajili.
Ninaposema UB inazidi kutanuka kwasababu wakati unafariki Dunia ukiacha
UB ikiwa na madarasa yake Eneo la Kawe Beach na Makao Makuu yake
Mikocheni kwa Warioba Dar es Salaam.
Lakini wanafunzi wapya waliojiunga Mwaka huu kwa idadi ya wanafunzi
imeongezeka ,uongozi wa Chuo umekodi jengo lililopo ndani ya eneo la
Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), linalomilikiwa na Kanisa hilo
Kinondoni Dar es Salaam ambalo jengo Hilo lilikuwa likitumiwa na Chuo
Kikuu cha Tumaini.
Ishara ya chuo hicho ulichokiasisi kimekua,UB imezidi kutoa ajira za
kudumu kwa walimu na watumishi wa Kada mbalimbali na ajira za muda kwa
walimu.
Desemba 7 Mwaka Jana ,Chuo Kilifanya mahafali yake ya kwanza Katika
ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na mwizi wa First Lady wako, Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohammed Ghalib Bilal ndiye
alikuwa mgeni rasmi na Kabla ya sherehe kuanza tulikukumbuka kwa
kusimama juu na kukuombea ikiwa ni Ishara ya kuthamini mchango wako kwa
UB.
Na Mungu akipenda Desemba 6 Mwaka huu, UB itafanya mahafali ya pili.Tuna
kukumbuka sana Kwani ulikuwa ni miongoni mwa wahasisi wa UB lakini
umefariki na hivyo kushindwa kuona ni jinsi gani chuo ulichokibuni na
kukianzisha wewe na Balozi Mahalu na wengine jinsi kinavyozidi kukua
kwa kasi.
Tukiachana na eneo la elimu ambapo Marehemu Dk.Mvungi alikuwa ni
Mwanataaluma kwa maana ni Mhadhiri wa fani ya Sheria na Mtetezi wa Haki
za binadamu.
Dk.Mvungi ,Septemba 26 Mwaka huu, Kituo Cha Utetezi wa Haki za Binadamu
(LHRC), kilifanya sherehe ya kutimizwa Miaka 19 tangu Kituo hicho
kilivyoanzishwa na miongoni mwa waasisi wa Kituo hicho ni wewe.
Aidha siku hiyo LHRC ilizindua Kitabu kilichobeba makala za
waandishi Mbalimbali ikiwemo makala yangu yenye kichwa cha habari '
Dk.Sengondo Mvungi ameniuma'.
Kila mwandishi wa makala zilizowekwa kwenye kitabu hicho ,alikuelezea
jinsi alivyokufahamu maisha uliyoishi hapa duniani na k kitabu hicho
kimepewa jina la ' Dk.Sengondo Mvungi , Breathing the Constitution'.
Katika Medani siasa Dk.Mvungi alikuwa ni Mwanachama wa muda mrefu wa
Chama Cha NCCR- Mageuzi ,Chama alichokipenda kutoka Moyoni na alijitolea
kwa Moyo wake wote kukijenga Chama hicho na kujitolea Fedha, mahalifa
ya fani yake ya Sheria na Katiba.
Licha ya Kuwa Mwana NCCR - Mageuzi hakuwa akiwachukia wanachama wa vyama
vingine. Dk.Mvungi aliamini Katika kumcha Mungu, siasa za kuvumilia
na kushimiana nakupenda siasa za vurugu.
Baada ya Dk.Mvungi kumaliza kampeni zake za kugombea Kiti Cha Urais
Mwaka 2005 ,mimi nilikuwa ni mwandishi wa kike peke yangu ambaye
niliungana na waandishi wa Kiume katika msafara wake wa kampeni
,alitueleza watu wake wa karibu Kuwa alipokuwa Akizunguka nchi nzima
Katika mikutano yake ya kampeni amegundua kuing'oa CCM madarakani siyo
kazi Rais Kama yeye na wanachama wa vyama Vya upinzani wanavyofikiri.
Dk.Mvungi alisema CCM imejiimarisha toka ngazi ya matawi Katika maeneo
yote kitendo ambacho ni tofauti kwa vyama Vya upinzani ambavyo hata
kwenye baadhi ya Kata hapa Dar es Salaam, havina Ofisi wala matawi na
Matokeo yake kila kukicha vyama Vya upinzani vimekuwa vikifanya siasa
zake kwa kutumia mikutano ya waandishi wa Habari wakati kwa CCM Hali
siyo hivyo.
Na kabla Kabla hajafariki alikuwa akiniambia mara kwa mara analiona
anguko la Chama Kimoja Cha Siasa Cha upinzani (sitakija kwa jina) Kwani
chama hicho kinafanya siasa zinazoambatana na vurugu na maandamano kila
kukicha na kwamba Watanzania ni watu wanaopenda Amani ipo siku
watakikataa kwa hoja kuwa Chama hicho ni Chama kinachofanya siasa kwa
vurugu na kushinikiza kufanya maandamano yasiyo na Kibali.
Na kweli utabiri huo wa Dk.Mvungi wa Miaka minne iliyopita Kwangu Mimi
nauona umetimia Kwani HIvi sasa Chama hicho Cha upinzani kinaonekana
kina wanachama ambao wanaamini kufanya siasa zinazoambatana na vitendo
Vya Uvunjifu wa Sheria na baadhi ya wanachama wake wamefikishwa Katika
Mahakama Mbalimbali wakikabiliwa na makosa ya kuingia kwa jinai, kufanya
mikusanyiko haramu na kukaidi amri halali ya Jeshi la Polisi.
Leo ninapokuandikia makala hii Dk.Mvungi huko uliko, lile jaribio
ulilokuwa ukitamani lifanyike Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 ambalo
wazo ilikuwa imeishaandaliwa Kuwa vyama vyote Vya upinzani viunganishe
Nguvu Katika uchaguzi ule kwa kusimamisha mgombea mmoja wa urais
,wabunge na madiwani .
Lakini mwisho wa siku ulinieleza wazo Hilo lilipofikishwa Katika masikio
ya Mwanachama mmoja wa Chadema ambaye Chama hicho kinamuamini mno na
kupokea ushauri wake wa kisheria ( jina naliifadhi) ,alilipinga wazo
hilo kwa nguvu zote na Kusema Kuwa kila Chama kiingie kivyake Katika
uchaguzi ule ambapo Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyeibuka Mshindi Katika
uchaguzi ule kwa kupata kura nyingi za ndiyo.
Hata hivyo Oktoba Mwaka huu, Vyama vinne Vya upinzani yaani Chadema,
NCCR, CUF vimeingia makubaliano ya kufanyakazi kwa kushirikiana na
kwamba Katika uchaguzi Mkuu Mwakani ngazi ya Kata, Jimbo na rais
watasimamisha mgombea ambaye ataonekana Kuwa anakubalika na watu Wengi
Katika eneo husika. Tusubiri Tuone Ushirika huo utadumu au laa.
Licha Tayari kuna taarifa za chini kwa chini zimeanza kuvuja Kuwa kuna
baadhi ya viongozi wa Chama Kimoja Katika ushirika huo kimekuwa
kikiwatuma makada wake kwenda kuwarubuni wanachama wa vyama vingine Vya
upinzani ambao wanakubarika Katika eneo husika Kuwa vyama vyao siyo
maarufu na havina Nguvu, hivyo waviame vyama vyao hivyo Vya upinzani
wajiunge na Chama hicho Cha upinzani Chenye wabunge Wengi ili Majina
Yao yaweze kupitishwa nawawe wagombea Katika nafasi za Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Desemba Mwaka huu na uchaguzi
Mkuu uliopangwa kufanyika mwakani.
Baadhi ya vyama vinavyofanyiwa usanii huu bado havijagundua Kuwa kuna
Chama Kimoja 'kinawageuza wanasesere', vikija kupata Habari lazima vumbi
litibuke.
Ningali nikikumbuka ulifariki wakati Tume ya Mchakato wa Katiba Mpya
iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba ikiwa Katika hatua ya
kuandika rasimu iliyotakana na maoni ya wananchi mliyoyakusanya nchi
nzima.
Tume hiyo ambayo ilifanyakazi zake kwa muda wa Miezi 18 na ilitoka na
rasimu ambayo pamoja na mambo mengi rasimu hiyo ilisema wananchi Wengi
walio hojiwa Walipendekeza kuwepo na serikali Tatu .
Rasimu hiyo ya Tume baada ya kukabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete, Kikwete aliipongeza Tume hiyo kwa kazi nzuri .
Baada ya Ripoti hiyo kumkabidhi kwa Rais na Jaji Warioba Kusema
kilichopo ndani ya Tume hiyo, wananchi wa Kada tofauti ambao waliisoma
na wengine hawakuisoma ila ni ushabiki tu waliibuka kila kukicha wengine
wakisema rasimu hiyo ni Mbaya na Haijazingatia maoni ya wananchi wote
na wengine Kusema rasimu hiyo ni nzuri.
Rais Kikwete aliteua wajumbe wa Bunge maalum la Katiba ambapo aliteuwa
watu wengi wakiwemo Balozi Mahalu na Dk.Natujwa kuwa wajumbe wa bunge
hilo na hivyo kufanya UB kuwa na wajumbe wawili katika Bunge hilo.
Bunge Hilo kilipoanza kazi yake lilikutana na Vituko Vingi ,malumbano
kutoka kwa Baadhi ya wanasiasa wa vyama Vya siasa,wanaharakati uchwara
,viongozi wa dini, vyombo vya habari ambao walikuwa wakirushiana
vijembe na uzushi wa kila aina na kutoleana lugha za kebehi na
kudhalilishana.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Oktoba 4 Mwaka huu, aliwatangazia
wanachama wa Chama Chake kote nchini waandae maandamano yasiyo na kikomo
bila ya kuomba kibali cha Polisi ,maandamano ambayo yalikuwa na lengo
la kushinikiza Bunge Maalum lisitishwe kwasababu lilichakachua mchakato
wa Katiba limedharau maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya Tume
ya Warioba.
Hata hivyo Jeshi la Polisi iliyapiga marufuku maandamano hayo kila
pande zote za nchi hii na waliokaidi amri hiyo walikamatwa na
kufikishwa mahakamani na hatimaye Bunge hilo likamaliza kazi yake na
Katiba Pendekezwa ikapatikana.
Lakini wakati Mbowe akisema hayo sijui alikuwa hafahamu Kifungu Cha 25
(2) Cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013 ambacho Kifungu
hicho kinatoa mamlaka kwa Bunge Maalum la Katiba kuongeza na kuboresha
rasimu (work document) yaani rasimu ya Tume ya Jaji Warioba wakati
walipokuwa wakiandika Katiba Pendekezwa.
Agizo Hilo la Mbowe lilikuwa ni dalili za wazi za kushindwa kuzuia bunge lile lisiendelee.
Kwani baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani wakiwemo wa chama Chako
Cha NCCR- Mageuzi,CUF, Chadema walisusia kikao cha bunge hilo kwa kile
walichodai kuwa wamechoshwa kudhalilishwa na wabunge wa CCM Katika Bunge
Maalum la Katiba na walijiapiza Kuwa akidi ya kura za kupitisha Katiba
Pendekezwa haitapatikana lakini ilipatikana wakaumbuka.
Na Mbaya zaidi baadhi ya wajumbe wenzio wa iliyokuwa Tume ya Warioba na
Warioba Mwenyewe nao wakati Bunge likiendelea nao walikuwa wakihutubia
kwenye midahalo na kuhojiwa na vyombo Vya Habari Kuwa akidi
haitapatikana lakini akidi ikapatikana .
Hata hivyo watu wako wa karibu ambao walikuwa ni wajumbe wa Bunge Maalum
la Katiba Kama mwanetu Balozi Mahalu ambaye alichaguliwa Kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Baadae Mahalu na Dk.Natujwa ,
Dk.Harrison Mwakyembe hawakususia Bunge Maalum la Katiba ,walikuenzi
wewe uliyekuwa miongoni wa Watanzania ambao walikuwa wanataka Tanzania
iandike Katiba Mpya lakini mtu wako mwingine wa karibu James Mbatia yeye
na wabunge wengine wa NCCR- Mageuzi walikuenzi kwa kususia kuhudhuria
vikao Vya Bunge Maalum la Katiba kuandika Katiba Pendekezwa ambayo kwa
zaidi ya asilimia 70 imetengenezwa kutoka na maoni ya Tume ya Warioba
ambayo wewe ulikuwa ni miongoni mwa wajumbe ambao mlizunguka nchi nzima
kukusanya maoni ya wananchi.
Kwa hiyo NCCR- Mageuzi ilikuenzi katika mchakato wa kuandika Katiba
mpya ambao mchakato huo ambao hivi sasa umefikia hatua ya wananchi
kuipigia kura za ndiyo au hapana Katiba Pendekezwa ambapo Tayari Tume ya
Taifa ya Uchaguzi imetangaza Kura ya maoni kuhusu Katiba Pendekezwa
itapigwa Aprili mwakani 2015.
Licha ya akidi kupatikana bado baadhi ya waliokuwa wajumbe wenzio wa
Tume ya Warioba walikuwa wakienda kwenye midahalo Kusema Katiba
Pendekezwa haina Afya na wakati wakiikandia Katiba Pendekezwa,
aliyesababisha wewe usiwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais
Kikwete ambaye tulikuwa tunamtani aliiba kura zako kwa maana hiyo wewe
ni 'rais Mdhurumiwa' na Rais wa Zanzibar, Dk.Mohammed Shein wamekuwa
wakiisifu wazi wazi.
Kuwa Katiba Pendekezwa ambayo imependekeza muundo wa serikali mbili
uendelee ni Katiba Bora na wanawashawishi wananchi waipigie kura na
kwamba hawana mashaka kuwa Katiba Pendekezwa itapitishwa na wananchi
wengi.
Dk.Mvungi Kama unavyonifahamu mini mwanamke jasiri ambaye usema kile
ninachokiamini hadharani, ukweli ni kwamba Katika uchaguzi wa serikali
za mitaa unatarajiwa kufanyika Desemba Mwaka huu na uchaguzi Mkuu
mwakani Dalili za wazi zinaonyesha kuwa vyama Vya upinzani vinaweza
kujikuta vikipoteza viti Vingi mno na majimbo mengi yakirudi CCM.
Kwa sababu hakuna wakati wowote ule ambao CCM imejipanga kimkakati NA kushinda kuliko vyama Vya upinzani.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulahman Kinana na Katibu wa Itikadi Unezi , Nape
Nnauye wanachanja Mbuga kwenda kuzungumza na wananchi kuimarisha Chama
'kusteamleti Chama ' .
Baadhi ya Viongozi wa vyama Vya upinzani wao Kutwa wapo Kwenye
midahalo wakitoa hotuba ya kupinga Bunge la Katiba, Katiba Pendekezwa na
Madai mengine ambayo hayana tija kwa vyama vyao zaidi ya kunufaisha
kundi Fulani.
Ila mume wangu wa zamani ambaye wewe umpora 'Mke' ambaye ni Mwenyekiti
wa Chama Cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, Mwenyekiti wa UDP,
John Cheyo walikuenzi kwa kukataa kususia Bunge Maalum la Katiba badala
yake walihudhulia vikao vyote Vya Bunge lile licha nao kila kukicha
walikuwa wakisakamwa na baadhi ya wabunge wa Chama CUF,NCCR- Mageuzi na
Chadema Kuwa ni wasaliti wa wananchi na wanafuata posho bungeni .
Ujinga mtupu Kwani tangu wapinge mchakato wa Katiba wametumia Rasilimali
nyingi na muda mwingi kupinga mchakato wa Katiba na hawa mafanikiwa na
wakati wakifanya hay, viongozi wa CCM walikuwa wakipita mikoani
kuimarisha Chama na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukijenga Chama chao
yake Makundi yaliyokuwepo Katika uchaguzi wa Mwaka 2010 ambayo
yalisababisha baadhi ya wana CCM Kuwaasaidia wagombea upinzani washinde
kwasababu Katika kura za maoni wagombea waliokuwa wakiwaunga mkono
walikatwa.
Walianzisha Operesheni 'Delete CCM, Operesheni Sangara Matokeo yake
Samaki Sangara hao wamechina kwasababu Kama wasingekuwa wamechina
,tungeona Matunda ya operesheni sangara na Kama kweli tungeshuhudia
CCM inatoka madaraka lakini wapi ndiyo kwanza CCM inazidi kustawi
Kama Shina la Mgomba.
Kinachonikera kwa vyama vyetu hivi Vya upinzani kweli kuna kazi nzuri
zinazofanywa na vyama hivyo,ila tu vyama hivi sijuii kwa kutokujua au la
wakati mwingine vikaamua kujiingiza kujadili masuala Fulani ambayo
hayapo Kabisa kwenye Kwani za vyama vyao au kutoa matamko ambavyo ni
Mwendawazimu peke yake anaweza kuyatoa.
Sasa Misielewi kampeni hizo zinazobeba ujumbe wa kuing'oa CCM ni
kampeni ambazo zinaandaliwa na wakubwa wa vyama hivyo pindi
wanapojisikia wanahamu ya kufanya utalii wa ndani ili wajiongezee
kipato kwa kisingizio Kuwa wanafanya ziara ya kuimarisha vyama vyao
mikoani au laa!
Bunge lile Maalum la Katiba licha lilikuwa likiundwa na wajumbe
walioteuliwa na Rais, pia wale wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nao pia walikuwa ni wajumbe wa Bunge lile ambalo bunge lile
lianza kazi zake Februali 18 hadi Oktoba 4 Mwaka 2014.
Dk.Mvungi kwakuwa baadhi ya wanachi walikuwa wamechoshwa na mwenendo wa
waliokuwa wajumbe wenzio wa Tume ya licha ya kukabidhi rasimu yao kwa
Rais Kikwete walianzisha Kama utaratibu wa Utendaji kazi wa lilokuwa
Bunge la Katiba na Katiba Pendekezwa.
Ndipo wNovemba 2 Mwaka huu, katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Taasisi ya
Mwalimu Nyerere ambapo kulikuwa na mdahalo wa Katiba ambapo mdahalo
ulivurugika na kuairishwa hadi siku isiyojulikana kutokana na kuibuka
kwa kikundi Cha watu kunyanyua mabango juu ambayo yalikuwa yameandikwa
ujumbe uliokuwa ukiunga mkono Katiba Pendekezwa.
Hali iliyosababisha wale ambao walikuwa hawataki kuyaona mabango hayo
kuanza Kupambana na hivyo kusababisha mdahalo kuvurugika na Mtani wangu
Warioba na kundi lake ambao ni waliokuwa wajumbe wa Tume yenu Profesa
Paramagamba Kabudi ambaye Katika Harusi yake wewe ulikuwa MC, Joseph
Butiku, Humphery Polepole kunusurika Katika vurugu hizo.
Ilikuwa ni hatari Tupu na Mtani wangu Warioba,hadi sasa hajasikika tena hadharani akizungumzia jambo la Katiba Pendekezwa.
Hata hivyo mwishoni mwa wiki Rais Kikwete alilazwa nchini Marekani na
kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume na anaendelea vizuri.Tunamuombea Mungu
apone licha kuna wengine wanakebei ugonjwa anaoumwa na Kuzusha magonjwa
Yao wanayoyajua wao.
Lakini Hao ndio 'Watanzania Proper' Tumeishawazoe Kwani wengine ni Kama wana roho za kichawi.
Mkeo Anna na watoto wako wote wapo salama wanaendelea vizuri na shule na
kazi. Na dereva wako Emmanuel amepata kazi ya udereva LHRC . Kwa ujumla
UB na LHRC inaendelea kuwatazama watoto wako.
Mimi nakuenzi 'Rais Mdhurumiwa ' Dk.Mvungi kwa kuendelea kuikamata elimu
na nimeamua kukuenzi kwa kuja kufanyakazi UB kama Afisa Habari na mzee
wangu Mahalu ili niweze kuja kuongeza nguvu.
Ila wakati mwingine nikiingia kwenye ofisi yako uliyokuwa ukikaa hapa UB, uwa nakukumbuka lakini sina jinsi.
Hadi sasa Mimi First Lady wako bado sijampata mume wa kuniona (
mgombea urais) hivyo uenda Katika kampeni za uchaguzi Mkuu Ujao ninaweza
kupata mume mpya baada ya wewe kuniacha Mimi Nikiwa mjane sina mtu wa
kunifariji na kunitunza licha walinzi wako uliowacha wananifuatilia
nyendo zangu.Teteteee
Mjukuu wetu Huyo mimi Bibi yake nimempa Majina mawili tofauti jina la kwanza Katiba na jina la pili ni Sengondo.
Nimempa Majina hayo kwasababu mama yake (Dk.Natujwa) akiwa na ukiwa na
ujauzito wa mjukuu wetu Rais Jakaya Kikwete alimteua Kuwa Mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba Hivyo akiwa na ujauzito huo Mtoto wetu mwingi
alikuwa akitoka Dar es Salaam kwenye kushiriki vikao Bunge Hilo ambalo
lilikuwa likiongozwa na Mwenyekiti wake Samwel Sitta.
Ndipo siku ya tarehe hiyo usiku ikiwa ni muda mchache baada ya kutoka
kwenye vikao Vya Kamati ya kuandika Katiba Pendekezwa ,mwanetu
Dk.Natujwa alijisikia uchungu anakimbiwa kwenye Hospitali hiyo na
kulifungua salama mjukuu wetu huyo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo( UB), Profesa Costa Mahalu ndiyo
aliyekuwa mtu wa kwanza kunipa Habari kuwa mwanetu Dk.Natujwa
ametuletea mjukuu na hivyo yeye (Mahalu) kuanzia Leo anaitwa Babu,
Mimi(Happiness) naïtwa Bibi na Natujwa anaitwa Mama.
Nilipokea kwa Furaha taarifa hizo lakini dakika Chache baadae nilipatwa
na huzuni nilianza kukumbuka na kutamani Mungu Angekupa Maisha Marefu
na wewe umone mjukuu wako wa kwanza Kwani nilipo mzaa Mwanangu Queen
'Malkia' na Kusema umefurahi kumpata Mkuu.
Nilijikuta natokwa Machozi ila sikuwa na jinsi nilimshukuru Mungu kwa kila jambo.
Binafsi nitaendelea ku kukumbuka Daima, Mema uliyotuasa tufanye sisi
vijana ambao tulikuwa karibu yako na kupata ushauri wa mambo mbalimbali
nitaendelea kuyapingatia licha siyo Siri kwamba tangu ufariki ule umoja
wetu wa vijana ambao tulikuwa tutafika ofisini kwako kupata ushauri na
kujadili masuala ya siasa umetoweka naweza Kusema nimebaki Mimi na kaka
yangu ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.George
Kahangwa ndiyo tunawasiliana.
Hata hivyo muda mfupi baada ya wewe kuzikwa ,watu wanaodaiwa Kuwa ndiyo
waliovamia nyumbani kwako na ku kushambulia kwa silaha za jadi Kama
kibaka ,walikamatwa na polisi na kufikishwa Katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa kosa la kukuua wewe kwa kukusudia
lakini hadi Leo upelelezi bado haujakamilika.
Aidha Dk.Mvungi bado Tanzania tuna Amani yetu bado tunayo haijavuriguka
na wale waliokuwa wakijaribu kutaka kuiburuga vyombo Vya ulinzi na
Usalama imekuwa ikiwadhibiti.
Niitimishe kwa Kusema leo ukiwa unatimiza mwaka mmoja tangu ulipofariki
duniani, nitakukumbuka Daima Kwani licha ya kuwa ' Mume wangu' , pia
ulikuwa ni mwalimu wangu Mzazi wangu. Pumzika kwa Amani.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blogg: katabazihappy.blogspot.com
0716 774494
Jumatano, Novemba 12 Mwaka 2014.
JIKUMBUSHE MAKALA YANGU YA MWAKA 2013
KIFO CHA DK.SENGONDO MVUNGI KIMENIUMA (2013)
Na Happiness Katabazi
NOVEMBA 12 mwaka 2013, saa 10 jioni nikiwa darasani katika Chuo Kikuu
cha Bagamoyo (UB) nasubiri mwalimu wa somo la Criminal Law aingie
kufundisha , mwanafunzi mwenzangu wa sheria ambaye ni Hakimu wa Mahakama
ya Wilaya ya Kinondoni, Marco Mochiwa alinifuata na kuniuliza mbona
watoto wa mwalimu wetu Dk.Sengondo Adrian Mvungi yaani Dk.Natujwa na
Nakundwa wamekuja kuchukuliwa ghafla na kurudishwa nyumbani.
Nilishtuka na kumwambia misijaona na nikamweleza Mochiwa kuwa taarifa
hizo alizonipa ni mbaya sana kwangu na licha sina ushahidi nazo natoka
darasani naenda ofisi ya walimu ilinikajue ni kwanini wamechukuliwa
hivyo kwani saa saba mchana nilionana na Dk.Natujwa chuoni hapo na
kuzungumza nae akasema kuwa baba yake hivi sasa anaitaji maombi kila
wakati na tuliongea mambo mengi sana ambayo siwezi kuyaandika katika
makala hii.Dk.Mvungi umeniuma sana.
Wakati nikishuka ngazi ghafla nikapokea simu toka kwa Mwandishi wa
Habari wa Gazeti la Mtanzania, Ester Mbusi akinipa pole ya msiba wa
‘mume wangu’ Dk.Mvungi.Niisii kuchanganyikiwa na kushuka ngazi pole pole
huku nikienda kwenye ofisi za walimu nikakuta zimefungwa na kwenda
kweny ofisi ya Meneja wa chuo,Innocent Mahedi na kumuuliza ni kweli
Dk.Mvungi kafariki na nikweli Dk.Natujwa kaondoshwa haraka chuoni hapo?
Mahedi alikatalia kata kata na kusema kuwa hana uhakika wa taarifa za
kifo hicho , nilimuuliza zaidi ya mara saba huku nikilia na kumuliza
iweje kama Dk.Mvungi ni mzima watoto wake wachukuliwe kwa dharula chuoni
hapo?Iweje kama taarifa hizo ni za uongo, waandishi wa habari wengi
wanipigie simu za kunipa pole zakuondokewa na ‘Rais Mdhurumiwa’? Mahedi
alijikausha ila niliwambia ukweli kuwa anafahamu ila ananificha.Kutokana
na mazingira hayo nilimpigia simu Dk.Natujwa alipokea na kusema hana
ushahidi na hilo ila wanaelekea Mwenge lakini nikasikia pembeni yake
kwenye simu analia sana anasema baba yake amefariki.
Siyo siri nilijikuta nikilia kwa sauti ya juu kwenye viunga vya chuo na
kukaa chini , namshukuru sana mwanafunzi mwenzangu wa sheria ambaye ni
mwandishi wa habari wa gazeti la The Citzen,Bernad James ndiye
aliyenisubiri nimalize kulia,na kuniinua kwenye mchanga nilipokuwa
nimekaa na kunibebea mkoba na kunishika mkono kuelekea kituoni ambapo ni
mwendo wa kama dakika 15 tukapanda wote Bajaji nanikamwambia kwakuwa
nimeambiwa wakina Dk.Natujwa wamepelekwa Mwenge nyumbani kwa marehemu
kaka yake Dk.Mvungi.
Nilianza safari ya kwenda hadi hapo Mwenge Kijijini saa 12 jioni na
nilipokelewa na wako wapi Dk.Natujwa wakanithibitishia ni kweli
Dk.Mvungi amefariki na watoto wake wamepelekwa Kibamba nyumbani kwa
Dk.Mvungi alikokuwa akiishi na mke wake Anna na msiba utakuwa
Kibamba.Nikapanda kwenye bajaji nalia sana hadi niliporudi nyumbani
Sinza saa moja usiku ndipo kidogo nilianza kukubali hali halisi kuwa ni
kweli ‘Rais Mdhulumiwa’ amefariki dunia, na kuanza kuandika makala hii.
Dk.Mvungi alijeruhiwa usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu kwa mapanga
kichwani na usoni na kusababisha kupoteza fahamu tangu siku hiyo na
Novemba 7 mwaka huu, alitolewa MOI na kusafirishwa kwenda Hospitali ya
Milpark nchini Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi lakini Novemba
12 mwaka huu, alifariki dunia.Dk.Mvungi umeniuma sana. Dk.Mvungi ‘Rais
Mdhurumiwa’ ambaye aliwahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, na hatimaye kufikia nafasi ya kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha
Chuo UDSM,ni miongoni mwa waasisi Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB) ambaye
kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katika na Rais
Jakaya Kikwete, alikuwa ndiye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Bagamoyo.
Kabla sijafika mbali napenda kutamka wazi kuwa kifo na ukatili
aliofanyiwa na wahuni ‘majini watu’, Dk.Mvungi yaliniumiza sana na
yanaendelea kuniumiza sana hasa ukizingatia Dk.Mvungi licha kilikuwa ni
chanzo changu cha habari ambaye alikuwa akinipa habari ambazo nyingine
nilikuwa naziandika kwenye gazeti na nyingine nilikuwa siziandiki kwenye
Gazeti alikuwa ni kama baba yangu wa kunizaa kwani aliniweka karibu
mno na familia yake,alikuwa akinishauri mambo mengi likiwemo la
kujiendeleza kielimu kwenda kusoma sheria, kifamilia, kazi yangu ya
uandishi wa habari hasa ukizingatia Dk.Mvungi aliwahi kuwa mwandishi wa
habari wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo licha hakuwai kusomea chuo
chochote kozi ya Uandishi wa habari.
Sitamsahau Dk.Mvungi katika hili ambapo mwaka 2009 niliomba kujiunga na
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kusoma kozi ya Cheti cha Sheria nikakosa
nafasi, nilivyokosa nafasi nilimfuata ofisini katika Shule ya Sheria
UDSM, na kumueleza hilo ambapo Dk.Mvungi alinitaka nimfuate anakokwenda
ili aende akawauleze ni kwanini mimi nimekosa nafasi ya masomo na fomu
zangu zilikuwa na dosari gani, tuliingia katika ofisi ya mhadhiri mmoja
anaitwa Semu Thomas ambaye alimsikiliza Dk.Mvungi na akamtaka Dk.Mvungi
arudi ofisini akakae na kwamba yeye Semu atabeba jukumu hilo na
alinipeleka hadi kwa Mkurugenzi wa Kozi ya Cheti cha Sheria Tairo,
ambaye alisikiliza na kulitatua tatizo langu na akanitaka nijaze fomu
upya, na kweli nilijaza fomu upya na zikagongwa mhuhuri wa uwakili na
Dk.Mvungi na hatimaye nikakubaliwa kujiunga na kozi hiyo.Dk.Mvungi
umeniuma sana.
Ndimara Tigambwage ndiye aliyemuingiza Dk.Mvungi katika fani ya uandishi
wa habari kwani Dk.Mvungi alikuwa akinielezaga kuwa hapa duniani kuna
watu anaweza kuwapinga adharani kupitia vyombo vya habari na siyo
Ndimara Tigambwage au Balozi Costa Ricky Mahalu. Kwani alipokuwa
amemaliza elimu ya kidato nne alikuwa akiishi kwa Marehemu kaka yake
Mwenge jijini Dar es Salaam, na wakati huo alikuwa akiandika mashahiri
na kuyatuma kwenye gazeti la Mzalendo na kuuza duka.Ndimara ndiye
aliyefika nyumbani kwa kaka yake Mvungi , Mwenge na kumshika mkono
Dk.Mvungi na kumpeleka katika gazeti la Mzalendo na kuwaomba wahariri
wampatie kazi ya uandishi wa habari ambapo alipatiwa kazi na
alifanyakazi katika gazeti hilo akiwa na rafiki yake ambaye naye ni
mjumbe wa Tume ya Mabadilko ya Katiba, Profesa Paramagamba Kabudi ambaye
naye pia hakuwai kusomea uandishi wa habari lakini alikuwa ni mwandishi
wa habari na mwisho wa siku Profesa Kabudi na Dk.Mvungi waliamua kwenda
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kusoma sheria na mwisho wa siku walifaulu
vizuri uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ukawapatia ajira ya
kuwa waadhiri wa sheria wa chuo hicho hadi miaka ya karibu Dk.Mvungi
alipostaafu utumishi wa serikali.
Dk.Mvungi pia alikuwa akinieleza kuwa hawezi kumpinga adharani Balozi
Mahalu kwani balozi Mahalu akiwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, ndiyo aliidhinisha Dk.Mvungi na wenzake waende
kuongeza shahada nyingine ya sheria nchini Ujerumani.Nakusema
anawaheshimu sana. Kweli maneno yanaumba.Mara zote Dk.Mvungi alikuwa
akimweleza mwanae mkubwa ambae ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu
cha Bagamoyo(UB), Dk.Natujwa Mvungi siku akifariki ,mkewe mdogo yaani
mimi Happiness Katabazi ambaye mara zote alikuwa akipenda kuniita ‘First
Lady’ nitaandika makala ambayo itamuelezea yeye alikuwa ni mtu wa aina
gani katika dunia hii na tulikuwa tukicheka Dk.Mvungi akisema hivyo na
mimi nikawa ninamwambia ata akifariki ghafla tayari nina picha zake
nyingi tulizopiga pamoja kwahiyo sitapata shida ya kutafuta picha zake
hizo na kweli limetimia.
Tangu nianze kuwa karibu na Dk.Mvungi kama mzee wangu mwaka 2000- 2013
,pamoja na mambo mengi alikuwa akinieleza kuwa enzi zaDk. Eliuther
Kapinga, mwaka 2002. Kapinga aliuawa kikatili kwa kunyongwa shingo na
kupigwa nondo kichwani nyumbani kwake, Mbezi Beach.
Katika ujana wake Dk.Mvungi alikuwa akinieleza kuwa alikuwa akipenda
sana kucheza mchezo wa ngumi na hadi hivi sasa Dk.Mvungi alikuwa
akifanya sana mazoezi ya viungo na muongozaji mzuri tu shughuli katika
sherehe na misiba. Na hata harusi ya Profesa Kabudi na mkewe ,ni
Dk.Mvungi ndiye alikuwa MC wa harusi hiyo. Si hivyo tu hata Chuo Kikuu
cha Bagamoyo ambacho kinatarajia kufanya mahafali yake ya kwanza tangu
kilipoanzishwa rasmi mwaka 2011, kilikuwa kimepanga Dk.Mvungi ndio awe
MC wa mahafali hayo lakini kwa bahati mbaya akakutwa na mkasa huo
uliosababisha afariki dunia.Dk.Mvungi ameniuma sana jamani. Itakumbukwa
kuwa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mwaka 2005.
Dk.Mvungi alikuwa ni miongoni mwa wagombea urais.Itakumbukwa kuwa
uchaguzi wa mwaka 2005 ulisogezwa mbele kwasababu aliyekuwa mgombea
mwenza wa Chadema, alifariki dunia.Katika raundi ya kwanza ya kampeni,
aliyekuwa mhariri wangu wa Gazeti la Mtanzania , Gabriel Athuman
alinipanga niongozane na Augustine Mrema (TLP)katika kampeni zake ambapo
nilizunguka na Mrema katika mikoa 15 kama mwandishi wa habari wa
mgombea urais kwa tiketi ya TLP. Tume ya ya Uchaguzi ikasimamisha
kampeni kwaajili ya kifo hicho, ilipokuja awamu ya pili ya kampeni,
Mhariri wangu Gabriel Athuman ambaye kwasasa anafanyakazi katika Ofisi
ndogo za CCM, Lumumba Dar es Salaam,aliniondoa kwenye timu ya Mrema
ambaye naye Mrema na mkewe Rose walikuwa wakiniita mimi ni First Lady wa
Mrema, na kunipeleka kujiunga kwenye timu ya mgombea urais kwa tiketi
ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye ni Dk.Mvungi.
Kweli nilikuwa ni mwandishi wa habari wa kike peke yangu katika timu ya
waandishi wa habari zaidi watano wanaume na tulifanyakazi yetu vizuri na
Dk.Mvungi akawa anajigamba mbele ya Mrema kuwa amemwibia mke yaani mimi
enzi hizo nikiitwa ‘First Lady wa Mrema’, na kwamba hivi sasa Happiness
ndiye mke wa Dk.Mvungi kwasababu tu mhariri wangu amenipanga mwandishi
wa kik kwenye msafara wake na jina hilo la First Lady liliasisiwa na
Dk.Mvungi na mkewe Anna katika msafara wake ambao tulizunguka mikoa yote
ya Tanzania Bara na Zanzibar akiomba kura kwa wananchi ili awe rais wa
Tanzania.
Lakini kura hazikutosha kwa upande wake , kura zilitosha kwa mgombea wa
CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye alitangazwa kuwa rais. Dk.Mvungi hakuwa
na kinyongo na Rais Kikwete kushinda naninakumbuka baada ya Dk.Mvungi
kumaliza kampeni aliathirika sana kiuchumi , sikumtupa nilikuwa naye
katika shida na raha kwani nilipokuwa nafika ofisini kwake mimi ndiyo
niligeuka kuwa mhudumu , karani mpokeaji wageni wake kwa kipindi hicho
chote ninachokuwa ofisini wake. Ilipofika katika kampeni za uchaguzi
mkuu wa wa Urais mwaka 2010, Dk.Mvungi hakugombea na mimi nikiwa
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, aliyekuwa Mgombea
Mwenza wa CCM, Dk.Mohammed Gharib Bilal aliiomba ofisi yangu iniruhusu
niingie kwenye timu yake ya kuripoti mikutano yake ya kampeni ambapo
tulizunguka nae mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar , na nilikuwa
mwandishi wa kike peke yangu na wanaume watatu. Kampeni hiyo ya Dk.Bilal
ambaye kwa sasa ndiye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, ilisababisha kwa miezi mitatu niwe mbali na Dk.Mvungi hali
iliyosababisha Dk.Mvungi kuwa ananipigia simu ya kunitania huku
akilalamika kuwa Dk.Bilal ametumia madaraka yake vibaya amempora ‘First
Lady wake‘ ‘Happiness), yaani mimi na kwamba anakusudia kumfungulia kesi
madai Dk.Bilal kwa kumpora mkewe. Baada ya kampeni za 2010 kumalizika
nikarejea mtaani na nikawa naona mara kwa mara na Dk.Mvungi na kumpatia
‘umbea'unaondelea mitaani nay eye ananipatia taarifa za hali ya kisiasa
nchini na huko mikoani walikokuwa wanazunguka wamepata maoni gani ya
wananchi.
Lakini ghafla nikamsikia mtu ambaye mimi na Dk.Mvungi tumekuwa tukimuita
kwa utani kuwa ni mwizi wa kura za Dk.Mvungi mwaka 2005 na kwamba
Dk.Mvungi ndiye alishinda kiti hicho cha urais ila kura zake ziliibwa,
yaani Rais Jakaya Kikwete kamteua Dk.Mvungi kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba. Sote vijana wake tulifurahia uteuzi huo na
kumtakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya na mara kwa mara
nimekuwa nikienda kumtembelea katika ofisi hizo za Tume. Mara baada ya
kuteuliwa tukawa hatuonani mara kwa mara kama zamani kwani alikuwa
akizunguka mikoni kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya.
Nilikuwa nikimtania kuwa namimi nakusudia kumshitakiwa Rais Kikwete
kwasababu amesababisha ndoa yangu na yeye isambaratike kwasababu tangu
apewe ofisi eneo la Posta Mpya karibu na Ikulu, sisi watu wa karibu naye
tumekuwa hatumuoni mara kwa mara kwani amekuwa amaliza muda mwingi
kwenye vikao vya tume na kusafiri mikoani kukusanya maoni.Tunacheka
baada ya kutaniana hivyo kishatunaendelea na majadiliano yetu.
Dk.Mvungi ameniuma. Kwa wanaomfahamu Dk.Mvungi watakubaliana na mimi
kuwa kama Taifa tumepoteza mtu aliyekuwa na mchango mkubwa sana hakika
wasomi wa kozi ya sheria na kozi ya Uongozi na Utawala ambao walikuwa
wakifundishwa na Dk.Mvungi,wale waliokuwa wakitetewa bure kesi zao
mahakamani na Dk.Mvungi watakubaliana namimi kuwa wahuni wale wamemuua
kikatiri na kinyama mpenzi wetu ambaye bado tulikuwa tukimuitaji. Baada
ya uchaguzi mkuu wa 2006, Dk.Mvungi alikuwa ananiambia ametikisika
kiuchumi hivyo ‘First Lady wake nisirubuniwe na mafisadi
nikamtelekeza.Na alikuwa akiniambia kuwa nimepata mume mwenye kichwa
kikubwa ambacho kina akili na kinafikiri sawa sawa.
Alivyorudi kufundisha UDSM kufundisha na nilipokuwa naenda ofisini nakaa
nae hadi wakati mwingine saa tano usiku na kisha dereva wake Emma
anamrejesha Dk.Mvungi nyumbani kwake Chuo tunamuamsha mke wake Anna
anamfungulia mlango na kisha anamwamuru dereva wake anirejeshe nyumbani,
nilikuwa nikimshuhudia Dk.Mvungi pamoja na kazi nyingine alikuwa
akiniambia anakiunda Chuo Kikuu cha Bagamoyo , kwani anautaalamu huo na
kweli alikuwa akiandaa chuo hicho akishirikiana na Balozi Mahalu mimi
nikiwa shahidi wa mchakato huo kwani wazo la kuanzishwa chuo hicho ni la
Mahalu na Dk.Mvungi na kweli walifanikiwa hadi chuo kikaanza
kufanyakazi. Kwa ufupi Dk.Mvungi muda wake mwingi alikuwa akiumalizia
kazini, kujisomea, kutoa ushauri wa kisheria kwa vyama vya
siasa,wananchi waliokuwa wakiito huduma hiyo na wengine walikuwa hawana
fedha za kumlipa alikuwa akiwatetea bure mahakamani,alikuwa ni mtu
mwenye fikra za kimageuzi,hakupenda madaraka yeye alikuwa akinieleza
kuwa anapenda kuwasaidia watu kupanga mikakati safi ili watu hao waweze
kupata madaraka,aliweka mbele maslahi ya wanyonge na hakuwa mtu mwenye
kuwa na tamaa ya fedha na siku zote alikuwa akisema yeye hatembei wala
kushika fedha,fedha zake kidogo alizokuwa nazo zinashikwa na mkewe
Anna.
Oktoba 29 mwaka huu,ndiyo ilikuwa ni siku yangu ya mwisho kukutana na
kuzungumza kwa zaidi ya saa tatu na Dk.Mvungi ofisini kwake Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na tulipiga picha za kumbukumbu ya yeye kuwa katika
ofisi hiyo mpya, nilipomtembelea ambapo nilifuatana na mdogo wangu
Michael Machali alisema yeye yupo kwenye Tume hiyo kwaajili ya
kukakikisha watanzania wanapata Katiba bora, na kwamba atatumia taaluma
yake ya Sheria ya Katiba kuiwezesha Tume ya Jaji Joseph Warioba
kufanikiwa na licha anaishi Kibamba ila anafika ofisini hapo saa 12
asubuhi na kuondoka jioni .
Kumbe ndiyo ilikuwa ni siku yangu ya mwanzo na mwisho ya kumuona na
kumsikia hapa duniani Dk.Mvungi.Dk.Mvungi umeniuma sana. Dk.Mvungi siku
hiyo alitueleza na mdogo wangu kuwa siyo kwamba hapendi kuchukua muda
mrefu kukaa na familia yake, bali dhamira yake imekuwa ikimtuma kutumia
muda mwingi kwenda ofisini kuwatumikia watanzania na mara zote alikuwa
akimsifu na kumheshimu Mwalimu Julias Nyerere kuwa Mungu alikuwa
amewaletea watanzania kiongozi mwenye maono.
Dk.Mvungi umeniuma. Dk.Mvungi hakuwa mtu anayependa makuu licha alikuwa
ni mtu aliyependa haki,kuwafundisha watu , ukweli na kusimamia kile
anachokiamini bila woga na unafki.
Katika miaka ya karibu Dk.Mvungi alikuwa akilalamika taaluma ya habari
imekumbwa na mmomonyoko wa maadili hapa nchini, kwani baadhi ya
waandishi wa habari na wahariri wao wamekuwa wakiandika habari ambazo
azisaidii sana maendeleo ya nchi isipokuwa kuandika habari zinazojadili
tuhuma ambazo wakati mwingine ni za uzushi tu kuhusu ufisadi wa kiongozi
fulani na kwamba hivi sasa baadhi ya waandishi wa habari za ufisadi
wamezigeuza kama ndiyo dini yao na mara zote akawa ananiasa na
kunifundisha jinsi ya kujiingiza kwenye uandishi wa aina hiyo.
Nafahamu kuna wanasiasa na mawakili leo hii watakuwa wanalia na kusaga
meno kwasababu ya kifo hiki , kwasababu tulipokuwa wakiitaji kuandikiwa
hotuba zao za kisiasa na kufundishwa jinsi ya kujenga hoja katika
mijadala mbalimbali , kuwasilisha hoja mahakamani walikuwa wakimfuata
Dk.Mvungi hata usiku wa manane na Dk.mvungi alikuwa akiwasaidia na hadi
leo wanasiasa hao wamekuwa na majina makubwa sana hapa nchini ila
sitawataja majina.Dk.Mvungi umeniuma.
Kwa wale waasisi wa mageuzi wa nchi hii ambao hivi sasa ni wazee,
hawawezi kumtaja Dk.Mvungi enzi hizo akiwa ni kijana mdogo ambaye
alikuwa akishiriki kikamilifu kupitia taaluma yake ya sheria katika
kuakisha Tanzania inaiingia katika mfumo wa vyama vingi. Mzee James
Maparara, Mabere Marando, Dk.Ringo Tengo na wengine wanajua hilo kipindi
kile wanaanzisha Taasisi ya TANLET, pia nimiongoni mwa waasisi
waliokisuka Kituo cha Kutetetea Haki za Binadamu(LHCR) na Baraza la
Habari Tanzania (MCT) kupitia taaluma yake ya sheria.Dk.Mvungi umeniuma.
Nalipongeza jeshi la polisi kwa hatua yake ya kuwakamata watu waliodai
kuwa ndiyo waliomsababishia kwa makusudi kifo ‘Rais Mdhurumiwa’.
Naomba jeshi la polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),
Dk.Eliezer Feleshi kufanya kazi yao ya upelelezi ,kukusanya ushahidi
thabidi na kuandaa mashitaka kwa uweledi na kisha kuwafikisha mahakamani
kwani endapo watakurupuka katika kuiandaa kesi hiyo ni wazi mwisho wa
siku washitakiwa hao watakuja kuachiriwa huru na mahakama. Dk.Mvungi ni
mwanasheria wa kwanza kuuwawa kinyama Hapa nchini ni Dk. Eliuther
Kapinga, mwaka 2002. Kapinga aliuawa kikatili kwa kupigwa nondo kichwani
nyumbani kwake, Mbezi Beach. Lakini mwisho wa siku polisi na ofisi ya
DPP walifanyakazi yao vizuri ambayo ilimshawishi Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ,Juxson Mlai kuwahukumu adhabu ya kifo.Nilipata fursa ya
kuudhuria kesi hii mwanzo hadi mwisho wake.Ilikuwa ni majozi wakati
washitakiwa hao wakijitetea kwani walikuwa wakieleza jinsi walivyoitoa
roho ya Kapinga.
Mwanasheria mwengine ambaye pia alikuwa Mhadhiri wa sheria Mwandamizi
wa UDSM ni Profesa Juani Mwaikusya ,Julai 14 mwaka 2010 naye alifariki
kikatiri kwa kupigwa risasi akiingia nyumbani kwake eneo laSalasala, na
hatimaye polisi ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa na kesi hiyo
ilifunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Nimalizie kwa kusema kuwa Watanzania kama taifa hivi sasa miongoni mwetu
wenye roho katiri na ambao mnafikiri mungu haoni ukatiri na madhira
mnaowafanyia waja wake,mbadilike. Acheni hiyo tabia kwani mnatuweka roho
juu wenzenu na kuanza kuishi kwa wasiwasi .Kubalini kuwa mungu yupo,
tena hajazeeka wala kupofuka macho na mungu wa siku hizi ni kijana
anatembea na IPAD ameiunganisha na Wireles na anafanya mambo yake kisasa
na analipa malipo hapa hapa dunia tena haraka sana, na nyie ipo siku
atawaadhibu pamoja na vizazi vyenu.
Laiti mngetambua umuhimu wa Dk.Mvungi hapa duniani aliokuwa nao
msingethubutu kumtendea unyama ule.Mmemuuzia na kumuua Dk.Mvungi lakini
nataka mtambue kuwa mtasababisha watu wengi waliokuwa wakimtegemea
kutokana na mchango wa kazi yake waathirike zaidi na wengine waondoe
kesi zao mahakamani kwasababu wamekosa wakili wakuwawakilisha mahakamani
bure.
Nchi hii hivi sasa badala ya watu kuumiza vichwa kubuni mambo ya
maendeleo kama kuanzisha viwanda vya kutengeneza magari, ndege,Laptop
sisi ndiyo tumekuwa vinara wa kubuni mipango mkakati na endelevu ya
kufanyiana vitendo vya kikatili vya kutupia majini kwa bei nafuu,
kumwagiana tindikali, kutekana na kujeruhiana kwa mapanga, kuzulia
uongo, fitna. Tabia hizi ni mbaya sana na zinatisha kwani wahalifu hawa
siku hizi wala hawakusubiri njiani wanakufuata nyumbani wanakufanyia
unyama. Mmekatisha kikatiri maisha ya Dk.Mvungi ambaye alikuwa
anategemewa na familia yake ikiwa ni pamoja na kuwalipia ada za shule
watoto wake, kumtunza mkewe Anna na kuwapa mwongozo wanae.Dk.Mvungi
ameniuma.
Dk. Mvungi ameacha mke na watoto watano. Alizaliwa Novemba mosi 1952.
Mwaka 1994 alitunukiwa Shahada yake ya Udaktari katika fani ya Sheria
katika Chuo Kikuu cha Hamburg, Ujerumani. Mwaka 1987 alipata Shahada ya
Uzamili ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); mwaka 1981
alipata Shahada ya Kwanza ya Sheria UDSM.
Dk. Mvungi hadi mauti yanamkuta alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha
Kutetea Haki za Binadamu (LHRC). Mmwaka 1995 hadi 2008 alikuwa Mtetezi
na Mtafiti Mkuu wa Sheria na Haki za Binadamu katika Mradi wa Kituo cha
Kutetea Haki za Wafugaji. Aliwahi kuwa wakili kutoka LHRC katika kesi ya
Kikatiba ya kutetea wananchi wa Kijiji cha Nyamuma. Mwaka 2000 hadi
2003 alikuwa Mkaguzi wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha
Makerere, Uganda na mwaka 2003 alishika wadhifa wa kuwa Mkuu wa Kitivo
cha Sheria UDSM.
Daima Dk.Mvungi nitakukumbuka kwa mambo mengi likiwemo pia vazi lako la
suti kwani nitofauti sana na aina ya suti zinazovaliwa na wanaume wengi,
ni wanaume wachache sana wanaovaa aina ya mtindo wa suti alizokuwa
anavaa Dk.Mvung na aina ya maisha uliyokuwa ukiishi.Vijana wako
umetufundisha mengi mazuri tutayafuata na mabaya tuyaacha.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena