Header Ads Widget

Responsive Advertisement

REST IN PEACE MUNA (Muna Obiekwe)

Naija
Kutoka Nollywood, story hazikuwa kwa siku ya leo, wengi huenda hawakuamini kutokana na uvumi uliokuwa ukienea mitandaoni kwamba muigizaji Muna Obiekwe amefariki, lakini huo ulikuwa uvumi ambao ulikanushwa, hii ilitokana na muigizaji huyo kuumwa kwa muda mrefu ambapo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la figo.
Staa huyo wa filamu za Nigeria  amefariki jana mchana akiwa hospitali jijini Lagos kutokana na ugonjwa huo wa figo.
Wasanii wenzake pamoja na ndugu zake walifahamu kuhusu ugonjwa wake, kuna wakati aliwahi aliwaambia marafiki zake kwamba amepanga kuandaa show ya maigizo ya jukwaani ili kupata fedha za matibabu na hakuwa tayari kutangaza ili watu wakusanye michango kwa ajili ya matibabu.
Mastaa mbalimbali wa Nigeria wameshtushwa na kifo cha msanii mwenzao na wengine kuandika kupitia mitandao ya kijamii.
 https://instagram.com/p/yBB_-2HvnR/

Post a Comment

0 Comments