Huyu ni kijana wa Kitanzania ambaye amejipatia Umaarufu wa Kupika Midundo ya Tofauti sana ya Muziki hapa Afrika Mashariki. Sappy amefanya kazi na Wasanii Kibao hadi sasa Kama Prezzo ambaye alimuundia ngoma ya Marry Marry na My Girl, Kafanya Kazi na Kaka Sungura Rabbit, Nazizi na Wasanii wengine Kibao wa Kenya.
Heshima Kubwa sana aliipata kupitia ngoma ya Budder than Most ya Redsun ambayo Remix yake alishirikishwa Mkali Demarco toka Jamaica na sasa Heshima ya Sappy kwa Tanzania imeongezwa na XO Ngoma kali toka kwa joh Makini akishirikishwa Baba Samantha GNako.
Akiongea na @DJHAAZU ndani ya Kipindi cha Dundo cha Mambo Jambo RadioMapema Leo Sappy ameelezea Historia yake hadi kuja Kufanya kazi na Weusi wasanii ambao anasema Alikuwa na ndoto ya kufanya nao Kazi toka kitambo sana.
Sappy alienda Kenya Kusomea Muziki akiaamini kuwa Muziki unahitaji Elimu zaidi ya ambavyo watu wanafikiria na Alivyoenda Kenya Kusoma akagundua kuwa Muziki Unavyofanywa Kenya unafanywa Kisomi Zaidi tofauti na Tanzania.
Katika Mazungumzo yake akatiririka Mengi haswa alivyokuwa akitamani Siku moja afanye Kazi na Vijana ambao anaamini Wanajitambua na wanajua wanachokifanya WEUSI
NAZIZI & SAPPY
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena