Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | TIBA YA MALARIA, KIKOHOZI KIKAVU NA TB

Mlingoti ni aina ya miti fulani ambayo ni mirefu sana kwa lugha ya kiingereza miti hii hufahamika kama ‘eucaliptus’. Asili ya mti huu ni Australia.

Miti hii ni kati ya miti mirefu sana yenye zaidi ya mita mia hamsini, mkoani Iringa miti hii hufahamika kama ‘miti ulaya’ na hutumika sana kwa kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya nyumbani kama mbao, kuni au papi za kuezekea nyumba.

Mti huu unatumika sana katika tiba hususani majani yake ambayo huaminika kuwa na uwezo wa kutibu kikohozi kikavu, malaria, pumu, matezi pamoja na kifua kikuu.


Pamoja na hayo, mti huu wa mlingoti pia husaidia kwa wale wenye ugonjwa wa kisukari, figo, baridi yabisi, kuhara damu, maradhi ya kinywa sambamba na mafua ambapo mhusika huvuta mvuke wa moto.

Mbali na hayo pia mti huu hutumika kuoshea vidonda, kuulia wadudu.

Post a Comment

0 Comments