Mkuu wa wilaya ya Rorya SAIMON KEMORI CHACHA amesikitishwa na baadhi ya kaya kutokuwa na vyoo jambo linalo changia kuwepo kwa mlipuko wa kipindupindu na baadhi kuwa na vyoo ambavyo havitumiki. Amebaini baadhi ya migahawa kutokuwa na sifa ya kutoa huduma ya chakula kwa kutokuwa na vyoo.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa agizo la kufungwa kwa migahawa hiyo hadi hapo wamiliki wao watakapo chimba vyoo vya kisasa.
Akikagua choo cha soko la Utegi amewataka wahusika kukikamilisha choo hicho ambacho kitasaidia wafanya biashara wa soko hill ambao kwa sasa wanajisaidia ovyo.
Pia ameshauri Halimashauri kujenga eneo la kukusanyia takataka ambazo kwa sasa zinarundikwa kwenye eneo la soko na dampo hilo limekuwa kero KWA wananchi hasa nyakati hizi za mvuo KWA harufu Kali inayotokana na dampo hilo
Picha na kituo cha HABARI na mawasiliano utegitelecomcentre
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena