Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RORYA ~ Mkuu wa Wilaya ya Rorya ahimiza kilimo cha Ufuta kama zao mbadala la biashara

Na Thomas Nkaina:::


Mkuu wa wilaya ndg SIMONI KEMORI CHACHA amewataka wananchi wa Rorya kulima zao la ufuta kwani ni zao ambalo soko lake ni la uhakika.
DC amewataka wananchi kutumia fursa hii kwani mbegu hizi za ufuta zilizoletwa na idara ya kilimo kutoka SUA Morogoro ni za mda mfupi na zinazaa sana kwahali hiyo kibiashara zinamnufaisha mkulima tofauti na zakienyeji tulizozizoea. 
Amewataka wananchi walio chukua mbegu hizi wazihudumie vizuri kwa kuzipalilia vizuri ilizitoe Mavuno mazuri nakuwasisitizia kuwa soko ni la uhakika halina tatizo aliyasema haya baada ya Kituo Cha Habari na Mawasiliano (Utegitelecom Centre) kumtembelea ofisini kwake.

Nae mkulima ndg CHARLES OWISO OKAMBO amempongeza mkuu wa wilaya ya RORYA kwa kuhamasisha kilimo cha ufuta na kuwafanya yeye na wenzake kuhamasika na kununua mbegu wameweza kulima shamba eka 2 ambalo wamelihudumia vizuri na limesitawi vizuri sana na kwa sasa wanamatumaini makubwa kwamba watapata mavuno mazuri na wanampango wa msimu ujao watalima zaidi ya eka 10 kwani ufuta unasitawi vizuri tofauti na watu walivyo tafsiri kwamba ufuta haustawi ukanda huu wa RORYA.

Amewataka wananchi wajikwamue kwa kulima ufuta ili waondokane na na wimbi la umasikini, Pia ametanabaisha kua mda huu ambao shamba la mifugo la utegi uzalishaji wa ng'ombe umepungua serikali iruhusu wananchi wafanye kulima mazao ya biashara kama ufuta ambao ni wa mda mfupi ambao hauta zuia kama shamba litakuwa linaendelezwa mda ukifika
Nae DAICO Ndg Kaokola amesema mbegu za ufuta zina patikana pale wananchi watakapo zihitaji na amesisitiza mda wa kucheza na umasikini umepitwa na wakati na kuwataka wakuluma kuchangamkia fursa hizi za zao la biashara la ufuta wapate manufaa.


picha na kituo cha HABARI na mawasiliano (Utegitelecomcentre)

Post a Comment

0 Comments