Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RORYA | Bangi sasa Basi Wilayani Rorya, DC Atoa Amri kwa Wahusika Kuacha Kilimo cha Bangi Mara Moja

Image result for BANGI
Mmea wa Bangi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya ndg Charles Chacha,Daudi Murumbe amesema wakati wa opareshen ya kutokomeza bangi wameshuhudia mashamba makubwa ya bangi ambayo yangeweza kua  mbadala wa kulima mazao ya chakula wanalima zao la bangi 

Amesisitiza kwamba kulingana na hali ya hewa iliyoko Rorya ni aibu kwa Rorya kuomba msaada wa chakula huku wananchi badala ya kulima chakula wanakazana kulima bangi na njaa kuendelea kuwa tatizo kwa swala la uzembe.

Kwaniaba ya mkuu wa wilaya ndg Daud Murumbe amesema watendaji kwa sehemu kubwa wamekuwa ni tatizo, kwani wamekuwa wakishirikiana na wananchi ambao sio waaminifu na kuendeleza migogoro kwa wananchi na hasa wale watendaji wanao fanyia Kazi maeneo ya nyumbani.


Pia amewataka watendaji kuhakikisha wamasimamia zoezi la kutokomeza zao la bangi katika maeneo yao na kama itabainika kuna wakulima wanalima zao hili la bangi na mtendaji yupo basi vyombo vya sheria vitawashugulikia watendaji hao bila kujali cheo chake katika eneo husika.

Pia amesema rorya kwa sasa ina maafisa ugani  wakutosha katika maeneo karibia yote ya Rorya na niwajibu watendaji na maafisa ugani kutoa elimu ya kilimo chenye Tija kwa wananchi wanaowaongoza.

Pia ndg Kaokola ambae ni afisa Kilimo na Ushirika wilayani Rorya akitoa mada katika kikao hicho amesema kwa kweli wilaya ya Rorya ina bahati ya mazao takribani yote yanasitawi vizuri sana kuliko maeneo mengine mkoani Mara, amesema Rorya mazao ya biasha kama vile ufuta,dengu,choroko ,pamba ,alzeti na mpunga ni mazao yanayostawi vizuri sana lakini watu hawako tayari kutumia fursa hizo na badala yake in kuzalisha migogoro isiyoisha baina ya jamii.


Akazungumzia skimu za chereche singida andaki,ochuna na irienyi ni skimu ambazo zikisimamiwa vizuri zingeweza kuzalisha mpunga mwingi na hata kuweza kulisha mkoa wa Mara na kuuza ziada nje ya Mkoa.


Wadau walio hudhuria kikao hicho walionyeaha kufurahia kikao hicho na kusema ni kikao kizuri sana kwa kumbushana majukumu kwa kila kiongozi na kutambua nafasi aliyo nayo katika jamii anayo iongoza.na wameahidi kufanya mabadiliko katika maeneo yao na kwenda na kasi ya serikali ya awamu ya tano.


#UtegiTelecomunicationCenter

Post a Comment

0 Comments