Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Nicola Colangelo mmiliki na muanzilishi wa kampuni ya Coastal Aviation afariki dunia

Image result for Nicola Colangelo
Kwenye sekta ya Aviation Tanzania kuna msiba mkubwa sana.Muanzilishi na mmiliki wa kampuni maarufu sana ya usafiri wa anga ya Coastal Aviation,Amicus Nicola Colangelo amefariki dunia.

Huyu ni mmoja wa wadau wakubwa sana wa "General Aviation" ambapo kampuni yake ilikuwa na zaidi ya ndege 30,nyingi aina ya Cesna206,Cesna 208 pamoja na Pilatus12(PC12) ambazo zilikuwa na "destinations" zaidi ya 42 Afrika Mashariki na Kati,huku makao yake makuu yakiwa Dsm.

Nicola ni mmoja wa wadau wakubwa sana wa usafiri wa anga na utalii,akiwa na ubia katika Hotel ya Slipway,Camps katika pori la Selous na Ruaha.Hakuna mtu aliyekuwa mtumiaji wa ndege ndogo za TB one kwenda maeneo yasiyofikika kwa barabara kama Kogatende,Behobeho,Siwandu,Likawage nk bila kutumia ndege hizi.

Nicola raia wa Italia aliyelowea Tanzania aliianzisha kampuni hiyo mwaka 1987 akiwa na ndege moja tu ndogo aina ya C206,akifanya safari zake kati ya Dsm na Selous Game Reserve.

Kwa sasa,Coastal Travel Safaris ndiyo moja kati ya kampuni kubwa za "Safari Tour".Ni bahati mbaya licha ya utajiri wote huo, Nicola amefariki bila kuwa na mtoto.

Sekta ya usafiri wa anga Tanzania, na huduma za mahoteli, watamkumbuka sana Nicola, mzee wa Coastal Steel pale Kipawa.

Binafsi nitamkumbuka Nicola, Mzungu janjajanja...
Pumzika kwa Amani Nicola...Uende salama!! Alama zako katika usafiri wa anga zitadumu kwa muda mrefu.
image.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpeg 
Hivi ndivyo mmiliki wa Slipway Hotel na kampuni zake nyingine ikiwemo kampuni ya ndege ya Coastal Aviation ndugu Nicola Colangelo alivyoagwa na wafanyakazi wake.

Toka Hotel ya Slipway mpaka viunga vya Ras Kutani-Kigamboni,Camps za Watalii katika pori la Selous na Hotel zake kule visiwa vya Mafia ilikuwa ni majonzi matupu.

Mtoni Marine Zanzibar mpaka CSI na maeneo yote alipokuwa amewekeza,ilikuwa ni vilio na kwikwi za huzuni.Wafanyakazi wake wote katika maeneo yote aliyowekeza,walitenga muda wa kukaa kimya na kufuatilia habari za mazishi yake huko kwao Italia.

Ilikuwa ni siku ya huzuni,katika picha wapo wazee walioanza kufanya kazi na Nicola akiwa hana utajili mkubwa.Hakuwahi kuwaacha eti kwa sababu amejenga hoteli kubwa ya kitalii na wao hawakuwa na elimu kubwa ya kuhudumia utalii,Nicola alienda nao,na leo ametangulia mbele za haki na wao wamebaki.

Kuna wapishi wake walioanza kumpikia chakula binafsi toka miaka ya 1970's wakiwa mabinti wadogo,mpaka leo ni wabibi lakini alikuwa nao pamoja.

Picha hizi ni muunganiko wa matukio,katika hotel ya Slipway,Uwanja wa ndege wa JNIA eneo la Terminal One zilipo ndege zake,Mafia na Selous.

Hivi ndivyo,Nicola alivyoagwa,mtu wa watu na mlowezi aliyewekeza kwa wazawa kwa moyo mmoja.

Pumzika kwa Amani Nicola.

image.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpegimage.jpeg

Post a Comment

0 Comments