Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Michezo | Man U Watembezewa Kichapo na Barca

Image result for manchester united vs barcelona international champion cup

FedExField, Washington DC huko USA ilishuhudia mtanange kati ya Manchester United na FC Barcelona ikiwa ni Mechi ya International Champions Cup na Barcelona kuibuka kidedea kwa Bao 1-0.
Dakika ya 31, Barca walipata Bao baada ya kuunasa Mpira wakati Man United wakishambulia na Lionel Messi kutumbukiza Pasi mbele ambayo Valencia angeweza kuinasa lakini akateleza na Mpira kumkuta Neymar aliegeuka haraka na kufunga.
Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Man United katika Mechi zao za Ziara ya USA katika matayarisho kwa kwa ajili ya Msimu Mpya.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Manchester United (Mfumo 4-3-3): De Gea; Valencia, Lindelof, Smalling, Blind; Pogba, Carrick, Lingard; Mkhitaryan, Lukaku, Rashford.
Akiba: Bailly, Jones, Rojo, Mata, Martial, Andreas Pereira, Young, Romero, Herrera, Shaw, Fosu-Mensah, Fellaini, Mitchell, Darmian, Tuanzebe, McTominay, Castro.
Barcelona (Mfumo 4-3-3): Cillessen; Semedo, Mascherano, Umtiti, Alba; Rakitic, Busquets, Alena; Messi, Luis Suarez, Neymar.
Akiba: Marlon, Pique, Denis Suarez, Turan, Iniesta, Vermaelen, Alcacer, Digne, Roberto, Vidal, Ortola, Samper, Douglas Pereira, Munir, Ezkieta.
REFA: Armando Villarreal
Manchester United – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles [5-2]
17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah [2-1]
20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup) [2-0]
23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup) [1-1, Penati 2-1]
26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup) [0-1]
30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo
2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin
8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup) 

Post a Comment

0 Comments