Nyanza Fc Ya Wekwa Sokoni.
Na:Kennedy Lucas-Manyara.
Klabu Ya Nyanza fc ya Mererani wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara inayoshiriki Ligi Daraja la pili Tanzania (SDL) ipo hatihati kumalizia raundi ya pili ya ligi hiyo baada ya uongozi kutangaza kuiweka sokoni kutokana na ukata wa fedha.
Akiongea na Mwandishi wetu katibu wa Nyanza fc Daniel Filbert Ndaikya alisema hatua hiyo imekuja baada ya juzi alihamisi Uongozi,wanachama wadau na bodi ya udhamini wa timu hiyo kukaa kikao kuangalia changamoto ambazo timu inapitia na hali ya kiuchumi ambapo waliazimia timu iuzwe baada ya kukosekana pesa ya kuiendeleza tena.
Alisema mpaka sasa wamepeleka barua kwa chama cha soka mkoa wa Manyara(MARFA),na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na bodi ya ligi kuwajulisha kuuza timu huku akiweka wazi kuwa endapo timu hiyo itashindikana kuuzwa basi itabidi ivunjwe.
"Mashabiki wako katika hali ya uzuni kwa sababu mkoa mzima timu ambayo ilikuwepo ligi daraja la pili ni hiyo ya Kwetu Nyanza sasa aijapata sapoti imebidi tuishie hapo umefika pale ambapo mkono umefikia manake ulitarajia timu iwepo na inaendelea kutengeneza madeni ambayo uwezi kuyalipa huko mbele utapelekana mahakamani kwenye viombo vya dola siyo jambo la kiungwana sababu mpira ni Passion ni furaha kama unasikia tena ni suala la ugomvi aipendezi" alisema Ndaikya.
Kuhusu kambi Ya wachezaji alisema ilivunjwa wiki mbili zilizopita ambapo wachezaji walitarajiwa kuanza kuingia tena desemba 10 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya Mzunguko wa pili ya ligi daraja la pili Tanzania (SDL) lakini kwa sasa kurudi tena kwa wachezaji kambini itakuwa ni vigumu sana huku akisema kuwa kuhusu wale ambao wanaidai timu endapo itafanikiwa mauzo basi watalipwa madeni yao na endapo itashindikana pia wataangalia ni jinsi gani kila mtu anapata haki yake.
Nyanza fc iko kundi D ya ligi Daraja LA pili Tanzania(SDL) ipo kundi moja na timu za Mashujaa fc,Milambo fc ,Jkt Msange,Area c United fc,na Bulyanhulu fc ikiwa nafasi ya Tano kwa alama 4 tofauti ya alama 6 tu mbele ya vinara wa kundi hilo Mashujaa fc yenye alama 10.

0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena