Baada ya Kuumbuliwa Hatimaye huu ndo uamuzi aliouchukua:: BREAKING NEWS !!! MISS MZEE AJIVUA TAJI LA MISS TANZANIA 2014, SASA MISS TANZANIA MPYA 2014 NI LILIAN KAMAZIMA.
Lillian Kamazima ndiye MISS TANZANIA 2014 Aliyekuwa
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili,
Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa
tatu, Jihhan Dimachk.
Sitti Abas Mtemvu amelivua taji
hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka
huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo
alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo
lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la
wizara husika kufuatilia ukweli wake. “Baada ya kutwaa taji la urembo la
Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea
maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye
barua hiyo. “Shutuma hizo zimeandikwa katika
vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi
ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena
bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu
natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.
“Napenda
niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo
nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo
wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali
za Taifa.
Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa
waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya
Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia
waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni
na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.” Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi.
“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa
mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa
uamuzi huo niliochukua.” Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi
wa pili, Lilian Kamazima.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena