Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI
wa zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’,
Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya
kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa siku kadhaa.
Amigo
alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa
upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote
kufanyika.
Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Amigo
alikuwa mmoja wa wanamuziki waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa
uaminifu mkubwa kwa miaka mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na
wenzake kadhaa kuanzisha Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na
JKT na kuwa Ruvu Stars Band.
Akiwa
Twanga Amigo akajijengea umaarufu wa aina yake na kuwa kama moja ya
nembo ya bendi, katika utumishi wake uliotukuka ndani bendi hiyo,
akafanikiwa kutunga wimbo mmoja 'AMINATA' ambao ulikamata chati kwa
miaka mingi tangu ulivyorekodiwa mwaka 2003.
Kufariki kwa Amigo ni pengo kubwa kwa Ruvu Stars hasa kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye alikuwa
‘injinia’ wa mipango yote kuanzia Super Stars hadi Ruvu.
Kabla ya Twanga Pepeta, Amigo aliitumikia pia bendi ya Bicco Stars chini ya Kinguti System.
Msiba uko nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu Mburahati jijini Dar es Salaam jirani kabisa na Shule ya Msingi Mianzini na taratibu za mazishi zinasubiri ndugu na jamaa kutoka Tabora na Kigoma
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena