Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MADAWA YANAZIDI KUTUTESA: Hiki ndicho kilichotokea Jijini Dar Es Salaam

Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo 40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi bilioni2.

 
Tukio hilo
lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifanikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.

Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitisha kuwa  kuwepo kwa tukio hilo huku akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.

“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo  lakini watu kama hawa siwezi kusema moja kwa moja ni Mchungaji ndie mhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha, kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara hii,”Alisema Nzowa.


Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka hadharani ukweli w
a mambo.

Post a Comment

0 Comments