Mitandao ya Zimbabwe imeandika kuhusiana na mchungaji Novert Chivese kukutwa akifanya mapenzi na mke wa afisa wa polisi msituni.
Stori ni kwamba, baada ya wawili hao
kukutana waliondoka ndani ya gari na kulekea kwenye msitu huo na
kuendelea na kitendo hicho ambapo askari polisi waliofika eneo hilo
walishtushwa baada ya kuona gari inatikisika kwa nguvu, baada ya kusogea
karibu ndipo wakabaini kinachoendelea baina ya wawili hao.
Mwanamke huyo Fortunate Safuri ameolewa
na Allen Tafirei ambaye ni askari wa idara ya Polisi ya Beatrice,
Zimbabwe ambapo wana zaidi ya miaka nane kwenye ndoa yao.
Baada ya kuwafuma waliwapeleka kituo cha
Polisi na kupigwa faini ya kiasi cha dola 20 kila mmoja kwa kosa la
kufanya mapenzi hadharani, japo hatma ya ndoa zao bado haijafahamika.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena