Ukiwa umesahau password yako au pattern ya simu janja, mara nyingi huwa tunapeleka simu kwa fundi ambae tunamjua atusaidie. Nimekuletea njia rahisi ya kufanya ‘Factory reset’ mwenyewe
Kabla ya yote, jua kwamba data na faili zako kama namba za simu, picha, apps na vitu vyote vitafutika baada ya kufanya factory reset. SwahiliBytes haitahusika na ufutaji huo, fanya kwa tahadhari.
Simu za Samsung
Hatua 1: Bonyeza kwa pamoja kwa sekunde 7
Sauti juu + Kitufe cha kuzimia + Kitufe cha nyumbani
Hatua 2: Zitakuja orodha mbali mbali, kwa kutumia vitufe vya sauti shuka chini hadi kwenye “wipe data / factory reset”
Hatua 3: Bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). Itakuja orodha nyingine, shuka chini kwa kutumia kitufe cha sauti na chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu.
Simu za Huawei
Hatua 1: Bonyeza Sauti chini + Kitufe cha kuzimia + Kitufe cha nyumbani kwa pamoja kwa sekunde 10
Hatua 2: Zitakuja orodha mbali mbali, kwa kutumia vitufe vya sauti shuka chini hadi kwenye “wipe data / factory reset”
Hatua 3: Bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). itakuja orodha nyingine chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu
Simu za Tecno
Hatua 1: Bonyeza Sauti juu + Kitufe cha kuzimia kwa pamoja hadi logo ya android itokee
Hatua 2: Ikitokea logo achia vitufe hivyo, na bonyeza tena mara moja bila kushikilia ‘Sauti juu + Kitufe cha kuzimia’
Hatua 3: itakuja orodha, shuka kwa kitufe cha sauti hadi kwenye “Wipe data / factory reset” na kisha bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). itakuja orodha nyingine chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu.
Simu za HTC
Hatua 1: Bonyeza Sauti chini, na bila kuachia bonyeza pia Kitufe cha kuzimia hadi logo ya android itokee
Hatua 2: zitakuja orodha mbali mbali, kwa kutumia vitufe vya sauti shuka chini hadi kwenye “wipe data / factory reset”
Hatua 3: kisha bonyeza kitufe cha kuzimia simu (power). itakuja orodha nyingine chagua “Yes — delete all user data”. Hapo itakua tayari imefuta kila kitu.
Simu za LG
Hatua 1: Bonyeza Sauti chini, na bila kuachia bonyeza pia Kitufe cha kuzimia hadi logo ya android itokee
Hatua 2: Logo ya android ikitokea, achia kitufe cha kuzimia simu janja hiyo, endelea kubonyeza Sauti chini kwa sekunde 2
Hatua 3: Bonyeza kitufe cha kuzimia simu mara moja, ikitokea skrini nyingine ya factory reset, achia kitufe cha hatua 2
Hatua 4: Tumia kitufe cha sauti chini kuchagua Yes
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena