MFANYABIASHARA namba moja kwa utajiri Afrika, Alhaji Aliko Dangote,
amevutiwa na kasi ya ujenzi wa kiwanda chake cha saruji, kinachojengwa
mkoani Mtwara.
Alisema kutokana na kasi hiyo, anaamini ujenzi utakamilika kwa muda
muafaka, na uzalishaji wa saruji kuanza Juni mwakani kama walivyopanga.
Akizungumza mkoani hapa juzi baada ya kupata maelezo ya ujenzi kutoka
kwa uongozi wa Kampuni ya Sinoma ya China inayojenga kiwanda hicho, na
kuangalia namna ujenzi unavyoendelea, Dangote alisema ameridhika na
hatua iliyofikiwa.
“Nina furaha maendeleo ya ujenzi ni mazuri, wanajenga kwa kasi kubwa,
naamini tutafikia malengo yetu ya kuanza uzalishaji ya saruji Juni
mwakani,” alisema Alhaji Dangote.
Pia, alisema kuwa kiwanda hicho kitaanza uzalishaji wake kwa kutumia
makaa ya mawe na watatumia nishati ya gesi, itakapoanza rasmi
kuzalishwa.
“Tutaanza kuzalisha kwa kutumia makaa ya mawe, hatujajua gesi itakuwa
inauzwa kwa shilingi ngapi kwa uniti moja ila ni vizuri pia kutumia
nishati ya gesi,” alisema.
Kwa mujibu wa makubaliano, mradi huo unatakiwa kukabidhiwa Juni 2015,
na kuanza uzalishaji, lakini kampuni ya Sinoma iliyopewa jukumu ya
ujenzi wa mradi huo, imeeleza kuwa watakamilisha ujenzi Aprili mwakani.
Credits HabariLeo
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena