Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Wakulima washauliwa kutumia Banki



Wakulima wameshauliwa kutumia banki ili fedha zao ziweze kuwa katika hali ya usalama ikiwa ni pamoja na kushindania mashindano mbalimbali yaliyoanzishwa na mabenki
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Benki ya NMB T awi la Tarime Amos Mubus kipindi akiongea katika sherehe za NMB Family zilizofanyika Musoma kwenye kumbi zaTembo  Beech kwa kuhusisha wanafamilia wa NMb  Tawi la Tarime.
Amos amesema kuwa Banki ya NMB imeweza kurahisha kazi kwa wateja ususani maeneo ya Vijijini kwa kuweka Matawi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha teknolojia mbalimbali kama vile kupata huduma za kibenki kupitia  Simu suala ambalo linaweza kumurahisishia mteja katika huduma anazoitaji bila kufika katika Kituo na kuwataka wakulima kutunza fedha katika banki
Aidha Meneja huyo wa Bank amewataka wazazi kuwafungulia akaunti za akiba kwa watoto pamoja na wanafunzi wa shule ili fedha hizo ziweze kutumika pale wazazi wanapo kumbwa na matatizo.
Katika sherehe hizo ziliambatana na Michezo ya  kuogelea, kukimbiza kuku watoto kwa wakubwa, kukimbia ndani ya Magunia, pamoja na Michezo mbalimbali huku zawadi zikitolewa kwa washindi kupitia familia hizo za watumishi wa Banki

Post a Comment

0 Comments