Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MUSOMA | Mama Aua Mtoto Kisa Samaki


Mtoto wa umri wa miaka mitatu amefariki dunia kwa kupigwa na mama ake mzazi kwa tuhuma ya kula mboga huko mkoani Mara katika mtaa waSonga mbele kata ya Rwamlimi nje kidogo ya Manispaa ya Musoma.

Mwanamke huyo amefaamika kwa jina la Hellena magwita ambapo inadaiwa mama huyo alimwadhibu mtoto wake kwakula mboga aina ya furu,baada ya kipigo hicho mtoto alilia hadi akapoteza fahamu na mwishowe kupoteza maisha.

Baada ya tarifa hizo tumezungumza na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa songambele Bwana Frasinsico Owoko ambapo amekiri kutokea kwa tukio hilo katika mtaa wake huo nanakusema motto huyo alifariki dunia kutokana na kupigwa na mama ake kisa kula mboga aina ya furu nakupelekea kupoteza maisha.

Mwenyekiti amesema kuwa nivyema wazazi wakawa makini huku akiaasa jamii kutoa taarifa mapema wanapokuwa wanaona matukio kama haya huku akisema kuwa asili ya mkoa wamara wamekuwa wakitumia hasira zao kutenda matukio kama hayo huku wakishindwa kujizuia na wanatakiwa kutambua kuwa mkoa wetu wa mara nikati ya mkoa ambao umekuwa na watu ambao wanahasira lakini wanashindwa kujuzia hivyo kupelekea matatizo kujitokeza.

Nae mmoja ya wanandugu hao amesema kuwa hakubaliani nakifo cha motto eti kafarikikwa mchango kwani ukweli unafichwa ndani yake hivyo wataendelea kuchunguza ilikufahamu ukweli wakifo cha motto huyo.

Aidha Mpaka sasa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mara kwa uchunguzi zaidi, ambapo tarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi tutakujuleetea

Post a Comment

0 Comments