Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Charles Mlingwa |
Mkuu wa mkoa wa mara Dr. Charles Mlingwa akijitambulisha kwa watumishi wa halimashauri ya wilaya ya Rorya aliwashukuru kwa ukamilishaji wa madawati na kusema tatizo la madawati sasa limekwisha ila vyumba vya madarasa ni tatizo haya toshi na kuwa na hatari ya madawati hayo kuharibika.amsema watendaji wa kata ,vijiji,wenyeviti wa vijiji na wadau wote wa maendeleo walioko nje na wapenzi wa wilaya ya rorya kushirikiana kusaidia kujenga vyumba vya madarasa na nyumba za waalimu ili kuweza kuondoa uhaba wa vyumba vya madarasa na nyumba za waalimu.akizungumzia swala la kilimo Dr charles amesema rorya kuna fursa za mazao ya biashara kama ufuta ,alizeti ,pamba na mazao ya mboga na matunda ambayo yanaweza kuletea wananchi uchumi kama wataalamu wa ugani watatoa elimu kwa wananchi na wananchi wakapata uelewa juu ya kilimo bora na chenye tija.
Mwananchi akichangia mada |
Nae mkuu wa wilaya ya rorya alimshukuru mkuu wa mkoa kwa kutoa semina kwa hao viongozi tofauti na wengi walivyo tegemea kwamba walidhani wanakuja kupokea amri .bali nikutoa semina ya nini watumishi wa serikali wafanye na kutambua wajibu wa kila mtu
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena