Header Ads Widget

Responsive Advertisement

CCM KAZI IPO MWAKA HUU | Kagasheki atoa tamko.

Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na waandishi wa gazeti hili, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Na Mpiga Picha Wetu.  
---
 Hofu kuhusu nafasi ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao inazidi kuongezeka baada ya mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki kukitabiria chama hicho tawala “kazi kubwa”, akisema hali ya sasa “siyo ile iliyokuwa nayo miaka mitano iliyopita”.
Kagasheki pia alikitahadharisha chama hicho dhidi ya kuzidi kukua kwa nguvu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akisema iwapo umoja huo utamchagua mgombea makini, CCM itakuwa na kazi ngumu.
Balozi Kagasheki, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kabla ya kujiuzulu kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi.
Kauli yake inaungana na za vigogo wengine wa CCM waliotahadharisha mwenendo wa chama hicho dhidi ya ongezeko la nguvu ya upinzani, akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, ambaye alisema rushwa inakimaliza chama hicho, na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambaye alisema kuwa chama hicho kisitegemee ushindi wa kishindo.

Post a Comment

0 Comments