 WANAWAKE wengi waliowazuri wa sura huwa wanapenda kuolewa na wanaume 
wabaya wa sura. Hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wenye sura nzuri
 hupenda kuolewa na wanaume wenye sura mbaya ili kulinda uzuri wao kwani
 wanaamini kuwa iwapo ataolewa na mwanaume mwenye sura nzuri, uzuri wake
 hautaonekana kwa watu kwani mwanaume pia ataonekana mzuri jambo ambalo 
litamupunguzia mwanamke kuonekana mzuri katika jamii. Hii ndio maana 
wanawake wengi wenye sura nzuri wanapenda kuolewa na wanaume wenye sura 
mbaya. Dr. Linda Mtaalamu wa masuala ya mapenzi na uhusiano anasema " 
Wanawake wengi wenye sura nzuri wanatabia ya kutaka waonekane kuwa ni 
warembo, jambo ambalo linawapelekea kuolewa na wanaume wenye sura mbaya 
ili waendelee kushine katika jamii".
Pia wanaume wenye sura mbaya wanapenda kuoa wanawake wenye sura nzuri ili kulinda hishima yao kwa kupitia wake zao. Kwahili ndugu msomaji naomba ujaribu kufanya uchunguzi wa kina kwa kuangalia wanaume wenye sura mbaya, utagundua kuwa wengi wao wanapenda kuoa wanawake wazuri na wengi wao tayari wameshaoa wanawake warembo. Je, kwa upande wa wanawake weusi; je, wanapenda wanaume wa aina gani? Na kwa upande wa wanaume weusi pia wanapenda wanawake wa aina gani? Pia na wewe kama unajitabua kuwa uko hivi au vile je, unapenda sweetheart wako aweje. Sasa tujadili.........................!!!!!

0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena