Habari zilizotufikia katika Mtandao wa Rorya Finest Blog kutoka
kwa mmoja wa wadau waishio Wilaya ya Temeke Jijini Dar, zinasema kuwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam limetumia mabomu ya
Machozi ili kuwatawanya Wafuasi na wapenzi wa Chama cha Wananchi CUF
waliokuwa wakiandamana kuelekea Mbagala kwaajili ya kuwakumbuka
wanachama wenzao waliopoteza maisha Huko Zanzibar Januari 26,2001.
Jeshi
hilo limefanikiwa kuwatia nguvuni viongozi waandamizi wa chama hiko
wakiongozwa na Mwenyekiti wao Taifa Prof Ibrahim Lipumba.
Akithibitisha
kukamatwa kwa viongozi hao pamoja na Mwenyikiti wao Afisa Habari wa
CUF, Bw Silas amekaririwa akisema Kuwa walianza maandamano ya amani
katika viwanja vya Temeke na Kuelekea Mbagala ambapo maandamano hayo
yaliyokuwa na lengo la kuwakumbuka wanachama wa CUF waliopoteza maisha
Januari 26 2001 katika maandamoo huko Zanzibar na Tanzania Bara.
Bw
Silas aliongezea kuwa wakati walipofika Mtoni Mtongani, Wilaya ya Ilala
Manispaa ya Temeke Jeshi la Polisi liliwasili na kuanza kurusha mabomu
ya machozi na Kuwapiga Wanachama na hatimaye kufanikiwa kuwatia nguvuni
viongozi waandamizi wa chama hiko na kuwapeleka kituo kikuu cha Polisi.
Sababu za kuwakamata wanachama wa CUF na viongozi wao huku sababu za
kukamatwa kwao zikielezwa kuwa ni kufanya maandamano bila kuwa na
kibali.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena