Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NEWS | SIKU YA WANAMKE DUNIANI MWAKA 2015 KUADHIMISHWA KIPEKEE JIJINI MWANZA.

Na George Binagi wa Mtanzania Media Blog
Miongoni Mwa wadau Katika Jiji la Mwanza waliokutana leo katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu. Kikao hicho kilihusiaha Wadau kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Vyombo vya Habari, Mashirika na Taasisi Binafsi.
Mipango, Mikakati na Vikao vya hapa na pale kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake dunia mwaka huu upande wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, imeanza huku wadau mbalimbali wakitakiwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya Kushiriki katika Maadhimisho hayo.
Katika Kikao cha Pili cha Maadhimisho hayo kilichofanyika hii leo katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wadau mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Vyombo vya Habari, Mashirika na Taasisi binafsi wakiwemo ambao wanaunda Kamati za Maadhimisho hayo wamekutana na Kujadiliana kwa pamoja namna ya kufanya ili Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani yaweze kufanikiwa vyema.
Mapendekezo mbalimbali yametolewa na Wadau hao, ambapo wadau mbalimbali wengine wameombwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya Kushiriki katika Maadhimisho hayo ambayo Kilele chake kinatarajiwa kufanyika March Nane Mwaka huu katika Kata ya Mirongo ikiwa ni katika ngazi ya Wilaya ya Nyamagana (Jiji).
Siku ya wanawake duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1911, wakati makundi ya wanawake nchini Marekani yalipokusanyika kupinga udhalilishaji, ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa kijinsia hususan katika sehemu za kazi.

Kuanzia wakati huo, Mataifa mbalimbali yalianza kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kupinga mfumo dume ambao uliwabagua wanawake kwa kuwanyima fursa za kusoma, kupata vyeo, mishahara mikubwa na haki ya kushiriki katika shughuli za maendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Vyama vya Wafanyakazi hapa nchini na duniani kote wamekuwa mstari wa mbele katika maadhimisho ya siku hii, ambayo kama nilivyotangulia kusema, kihistoria chimbuko lake limetokana na wafanyakazi wanawake kupigania haki zao.

Siku hii inatoa fursa kwa wanajamii, wafanyakazi wanawake, taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za kiserikali kufanya tathmini juu ya masuala mbali mbali ya kimaendeleo kwa wanawake na hasa kuangalia matatizo yanayowakabili na jinsi ya kuyatatua, kutafakari juu ya haki zao katika ajira na jamii, kufanya tathmini juu ya mafanikio yao na kupanga mikakati mipya ya kimaendeleo. Lengo kuu ni kuondoa vikwazo kwa wanawake katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii ili kujipatia maendeleo.

Aidha, madhumuni ya maadhimisho haya ni kupima utekelezaji wa Maazimio, Matamko na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayohusu masuala ya wanawake.
Miongoni Mwa wadau Katika Jiji la Mwanza waliokutana leo katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu
Baadhi ya wadau Katika Jiji la Mwanza waliokutana leo katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu.
Kulia ni Costansia Mbogoma kutoka Shirika la CAPACITAR TZ, akifuatiwa na Gloria Isack (Katikati) ambae ni Volunteer Kata ya Nyamagana na Kushoto ni Asha Mohamed Mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Mwanza.
Miongoni Mwa wadau Katika Jiji la Mwanza waliokutana leo katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu
Kulia ni Vervas Evodius kutoka Shirika la HAKIZETU akiwa na Winifrida Kaheshi (Kushoto) Kutoka Shirika la WOTESAWA Mkoani Mwanza.
Miongoni Mwa wadau Katika Jiji la Mwanza waliokutana leo katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu
Kushoto ni Dicksoni Sija Kutoka Shirika la NACOPH akiwa pamoja na Rahel Zakayo (Kulia) kutoka Shirika la ACORD.
Miongoni Mwa wadau Katika Jiji la Mwanza waliokutana leo katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu
Mwenyekiti wa Kikao (Kushoto) pamoja na Katibu wa Kikao cha leo (Kulia). Ilikuwa katika Kikao cha pili cha Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kuadhimishwa March Nane Mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments