Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LASITUSHWA NA WANASIASA NCHINI TANZANIA.

Peter Ash Kulia) kutoka nchini Canada ambae ni Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, Under The Same Sun. Mkutano huo umefanyika Mapema hii leo Ryan's Bay Hotel Jijini Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo nchini Tanzania Vicky Ntetema.
Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi Under The Same Sun limeelezea kushitushwa kwake na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa hapa nchini
kutoonesha mchango wao katika kupambana na mauaji ya Watu wenye Ulemavu wa ngozi.
Peter Ash ambae ni Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kutoka nchini Canada ameyasema hayo jana Jijini Mwanza, wakati akiongea na waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Ash amebainisha kwamba katika nyakati tofauti ambazo amekuwa akifika hapa nchini amekuwa akikutana na matukio mengi ambayo bado yanawasibu watu wenye ulemavu wa ngozi, matukio ambayo ni pamoja na kutekwa, kujeruhiwa na hata kuuawa kwa watu hao wenye ulemavu wa ngozi.
Amesema jambo linalomsikitisha zaidi ni kwamba, Katika matukio ya kutekwa, kujeruhiwa ama kuuawa kwa walemavu wa ngozi, viongozi wa kisiasa wamekuwa hawajitokezi kusaidia jitihada za kukomesha matukio hayo ama hata kushiriki katika kuwafariji ndugu wa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakikumbwa na matukio mbalimbali ya kikatili.
Ash ametolea mfano tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana la Kutekwa kwa Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Pendo Emmanuel katika Kijiji cha Ndami Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ambapo amesikitishwa na Viongozi wa Kisiasa akiwemo mbungwe wa Kwimba kutofika katika familia ya Mtoto Pendo kwa ajili ya kuwafariji akiwa kama kiongozi wao.
Katika hatua nyingine Ash amesikitishwa na namna watu wenye ulemavu wa ngozi wanavyowindwa hususani katika nyakati za Uchaguzi, ambapo amekemea vikali hali hiyo kuzidi kuendelea na amewataka viongozi wote wa kisiasa kutoa ushirikiano wao kwa lengo la kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Katika hatua nyingine Peter Ash amewataka watu wanaojihusisha na Ununuzi wa Viungo vya Watu wenye Ulemavu wa ngozi kufikishwa mahakani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria, badala ya Waganga wa Kienyeji pamoja na watu wanaotuhumiwa kufanya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi pekee kuwa ndio wanaofikishwa mahakamani.
Mkurugenzi wa Shirika hilo la Under The Same Sun nchini Tanzania Vicky Ntetemwa amewataka Watanzania na wadau mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano wao katika kuwafichua watu wanaojihusisha na ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni pamoja na kuwafichua watu wanaofadhiri vitendo hivyo ambapo amebainisha kuwa anaamini siku moja wale wote wanaodhani wana nguvu ya kifedha ama kisiasa wanaojihusisha katika Ukatili kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi ipo siku watabainika na watafikishwa Mahamakani.
Peter Ash Kulia) kutoka nchini Canada ambae ni Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, Under The Same Sun. Mkutano huo umefanyika Mapema hii leo Ryan's Bay Hotel Jijini Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo nchini Tanzania Vicky Ntetema.
Waandishi wa Habari (Wa kwanza kushoto na alie katikati) Mkoani Mwanza walikiwa katika Mkutano baina yao na Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, Under The Same Sun. Mkutano huo umefanyika Mapema hii leo Ryan's Bay Hotel Jijini Mwanza. Kulia ni Mmoja wa Watu wenye Ulemavu wa ngozi waliokuwa katika Mkutano huo.
Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza walikiwa katika Mkutano baina yao na Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, Under The Same Sun. Mkutano huo umefanyika Mapema hii leo Ryan's Bay Hotel Jijini Mwanza.
Miongoni mwa Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza waliofika katika Mkutano baina yao na Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, Under The Same Sun. Mkutano huo umefanyika Mapema hii leo Ryan's Bay Hotel Jijini Mwanza.
Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza wakiwa katika Mkutano baina yao na Muasisi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Watu wenye Ulemavu wa Ngozi, Under The Same Sun. Mkutano huo umefanyika Mapema hii leo Ryan's Bay Hotel Jijini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments