Je unafikiri ni iPhone au Samsung ndio wametengeneza simu zilizouzika zaidi? Soma hapa kuzitambua simu 20 zilizouzika zaidi katika historia.
Tutaanza na ya 20 kwenda hadi ya kwanza,
Namba 20: Nokia 3100 (3120)
Ilitolewa Mwaka: 2003
Idadi ya Mauzo: Milioni 50
Namba 19: iPhone 5S
Ilitolewa Mwaka: 2013
Idadi ya Mauzo: Milioni 52
Nafasi ya 18 inashikiliwa na Samsung kupitia Samsung Galaxy S III
Namba 18: Samsung Galaxy SIII
Ilitolewa Mwaka: 2012
Idadi ya Mauzo: Milioni 60
Namba 17 inarudi kwa Apple kupitia iPhone 4S iliyoingia sokoni Oktoba mwaka 2011, ilifanikiwa kuvunja rekodi ya kimauzo ya haraka kwa iphones kutokana na kufanikiwa kuuza zaidi ya milioni 5 ndani ya siku 5, milioni moja ikiwa ni malipo ya ndani ya masaa 24 kabla ya simu kuingia sokoni rasmi (pre-order). Pia mwanzilishi mashuhuri wa kampuni ya Apple, Steve Jobs, alifariki siku moja baada ya ujio wa iPhone 4S kutangazwa rasmi.
Namba 17: iPhone 4s
Ilitolewa Mwaka: 2011
Idadi ya Mauzo: Milioni 60
Namba 16 inashikiliwa na StarTAC kutoka Motorola! Muhimu hapa ni kwamba StarTac iliyotoka mwaka 1996 ndiyo simu ya kwanza kununuliwa kwa wingi duniani. Na kwa kuingia sokoni mwaka 1996 inakuwa ndiyo simu ya zamani zaidi katika orodha hii, na hii ndiyo simu ya kwanza kabisa kuwa ya kufunga (Flip).
Namba 16: StarTAC
Ilitolewa Mwaka: 1996
Idadi ya Mauzo: Milioni 60
Namba 15 inashikiliwa na simu kutoka Motorola tena, nayo ni Motorola C200. Haikuwa na mvuto sana, ila iliuzika! Nakumbuka kuziona simu hizi miaka ileeee.
Namba 15: Motorola C200
Ilitolewa Mwaka: 2006
Idadi ya Mauzo: Milioni 60
Nokia 5130 (5220/5310) inashika nafasi ya 14, na naamini ata wewe utakuwa unakumbukumbu nayo hii. Kama si wewe mwenyewe kutumia basi uliiona kwa sana. Ilipata umaarufu zaidi kutokana na uzuri wake na uwezo wake mzuri kwenye utumiaji wa intaneti na kusikilizia muziki. Ikiwa na sifa zile zile Nokia walitofautisha maumbo kwa matoleo ya 5220 na 5310.
Namba 14: Nokia 5130
Ilitolewa Mwaka: 2007
Idadi ya Mauzo: Milioni 65
Nafasi ya 13 inabebwa na Nokia tena, na hii ni kupitia Nokia 6010 (6020/6030) iliyotoka mwaka 2004, na hii ni moja ya simu ambayo hata kwetu ilitumika sana enzi zile.
Namba 13: Nokia 6010
Ilitolewa Mwaka: 2004
Idadi ya Mauzo: Milioni 75
Nafasi ya 12 inashikiliwa na iPhone 5 kutoka Apple, hii iliingia sokoni mwaka 2012. iPhone 5 ilikaribisha mabadiliko makubwa kufananisha na matoleo ya nyuma ya iPhone kama iPhone 4 na zinginezo, hii ilikuwa ni pamoja na kupata kioo kikubwa zaidi na pia mabadiliko ya utumiaji wa waya wa kuchajia.
Namba 12: iPhone 5
Ilitolewa Mwaka: 2012
Idadi ya Mauzo: Milioni 91*
Namba 11 inashikiliwa na Nokia 1208 (1209) iliyoingia sokoni mwaka 2007. Hii ni maarufu kweli, mwenyewe nishawahi itumia na nina uhakika vijana wa miaka ya 2008-10 wote watakuwa wameitumia au kuiona. Ingawa haikuwa na sifa za kisasa zaidi wengi waliipenda kutokana na uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu na pia uwepo wa tochi ya bure.
Namba 11: Nokia 1208
Ilitolewa Mwaka: 2007
Idadi ya Mauzo: Milioni 100
Je ushawahi kutumia simu ipi kati ya hizi tulizozipitia?
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena