Familia za ndugu wa watu waliopata ajali kwenye ndege ya TransAsia Airlines GE235
ambayo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege
Taipei, wamekutana na uongozi wa Kampuni hiyo jana na kujadili mambo
kadhaa ikiwemo malipo ya fidia na rambirambi za marehemu waliofariki
katika ajali hiyo.
Liu Zhongji
ni mwakilishi wa Kampuni hiyo ya ndege Taiwan, ametoa maelezo kuhusu
kilichozungumzwa katika kikao kilichokaa zaidi ya saa tatu ambapo
wanafamilia hao wamekataa kulipwa jumla ya dola milioni 14.9 za Taiwan
(zaidi ya Ths. Milioni 850/-) ambayo wangepatiwa ndugu hao kwa kila mtu
mmoja aliyefariki kwenye ajali hiyo.
Kiasi hicho cha pesa kilipangwa kutolewa kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi pamoja na rambirambi kwa wafiwa hao.
Ajali hiyo ilisababisha kifo cha watu
42, wengine 15 walifanikiwa kutoka salama huku mwili wa mtu mmoja ukiwa
bado unatafutwa, ajali hiyo ilitokea muda mfupi baada ya engine ya ndege
hiyo kupata hitilafu na kuifanya ndege hiyo kupoteza mwelekeo, ikagonga
ukingo wa daraja na kuanguka mtoni.
Janga lingine limewakuta marubani wa
Kampuni hiyo ambapo baada ya ajali hiyo kutokea walilazimika kuwapa
mtihani uliofanya 29 kati yao kusimamishwa kazi baada ya kufanya mtihani
huo uliowapima namna wanavyoweza kupambana na kuokoa ndege iliyopata
dharura.
Hii ni taarifa ambayo iliripotiwa kuhusu ajali hiyo FEBRUARY 4 na kituo cha CNN
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena