ya wadau wa sanaa wakiona msanii anakazi nzuri au kali kushinda kazi yao au ya mtu wao hawapo hawapo tayari kuipa support kazi hiyo kwa kuhofia kumzima mtu wao au msanii huyo kuhofia kupotezwa.Baraka amefunguka hayo alipoongea na www.eatv.tv
Mkali huyo wa miondoko ya RnB ambae kwa sasa anazidi kutoboa na ngoma yake ya Siachani nae ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya wasanii aliwapa kazi yake na kuwaomba kumpa
support lakini hata walivyokuwa wakiipokea kazi hiyo walionyesha hofu na hawakuweza kumpa suport ambayo aliihitaji.
"Wasanii wa bongo fleva kuna baadhi wanamapenzi ya kweli na nia ya muziki wetu kufika mbali hivyo wasanii hao waliweza kunipa support hata ya kupost ujioa wa wimbo
wangu na Cover lakini kuna wasanii nilipokuwa nawaomba wanipe support walikubali lakini baada ya kuwatumia wimbo hawakuweza hata kunipa support najua wengine walikuwa
na hofu kwa kuona wimbo ni mzuri hivyo labda walikuwa wanaogopa ninaweza kubeba mashabiki zao"
Baraka alizidi kuonyesha kuwa katika tasnia ya bongo fleva upendo kati ya wasaniii bado upo chini ingawa anaona kuna mabadiliko na huenda ipo siku wasanii watabadilika
na kuwa na malengo ya kufika mbali zaidi kwa kupeana support ya kutosha ili kuzidi kukuza muziki wa Bongo fleva nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika mashariki.
"Kama wasanii wote tungekuwa na upendo na kupeana support ya kweli hakika muziki wetu ungefika mbali sana tena kwa haraka mno lakini tatizo kuna baadhi ya wasaniii
pamoja na wadau wa sanaa unapofanya kitu kizuri sana hawakupi support kwa hofu zao wenyewe,lakini mimi naamini kama msanii kafanya kitu kizuri na sisi wote tuka
support inamaana hicho kitu kitaweza kufika mbali sana kwa muda mfupi"
Baraka Da Prince kwa sasa kupitia wimbo wake wa Siachani umeweza kupenya katika nchi mbali mbali ikiwepo Canada na nchi za Afrika Mashariki.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena