Serikali jijini Dar es Salaam imetoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa dalili za kufumuka kwa ugonjwa wa Dengue katika kipindi hiki cha mvua, huku ikiwataka wananchi wanaoishi mabondeni kuhama maeneo yao ili kunusuru maisha yao.
Akizangumza na waandishi wa habari leo , Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadiki amesema katika kuelekea kwenye kipindi cha mvua mwezi huu magonjwa mengi hutokea kutoka na kuongezeka kwa mazalia ya mbu na uchfunzi wa mazingira hivyo wananchi wanatakiwa kujianda kwa lolote
“Hakuna mtu asiyetaka mvua, mvua ni neema na sasa tunaelekea kwenye kipindi cha mvua, kipindi hiki huwa kinaambana na milipuko mbalimbali ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa Dengue kwa ajili ya maji kuhama na kutengeneza mazingira ya mbu, hivyo natoa wito kwa wananchi kutunza mazingira yao.” Amesema Meck Sadiki
Meck Sadiki ameongezea kuwa mbu anayeendeza ugonjwa huu hatari wa Dengue anapendakuishi na kuzaa kwenye maji jaliyohifadhiwa kwenye ndoo, mapipa , tenki, vyungu vya maua na pindi wanapozaliana kwa wingi husababisha maambukizi.
“Dalili za homa ya Dengue zinasababishwa na virusi vinavyoambukizwa kupitia mbu huyu aina ya ‘aedes egptian’ na husababisha homa kali, kuumwa kichwa , misuli na viungo mara kwa mara pia mgonjwa huwa na kichefuchefu wakati wote.”amesema Meck Sadick
Ametoa wito kwa wananchi kusafisha mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu, na kutangaza kuwa utupaji wa taka ovyo ni marufuku maana hizo taka zinachangia mitaro kuziba na maji kuhama, na kuongeza kuwa watu wote wanatakiwa kuepuka mikusanyo isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo ndefu.
Meck Sadiki amewataka wananchi kutumia vyandarua vilivyo tiwa dawa na kuweka wavu na kuzuia mbu katika madirishani yao, ikiwa ni pamoja na wale wananchi wanaoishi mabondeni kuhama haraka maeneo yao kwani ni hatarishi Zaidi kwa mazalia ya mbu.
Mwananchi.com
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena