Header Ads Widget

Responsive Advertisement

ARE WE ALONE IN THIS WORLD? Part two | TUKO PEKE YETU KATIKA ULIMWENGU HUU? Sehemu ya pili


Kuonekana kwa UFO kwenye anga la sayari yetu ya dunia siyo jambo jipya na geni. Katika kumbukumbu nyingi za kale kumekuwa na rekodi za vyombo mbalimbali vya kusafiria vya kale ambavyo vilikuwa na sifa za kupaa kama gari za angani, diski zenye mbawa, ndege na vyombo vingine vya angani vyenye mwanga mkali.




Jacques Vallee mtafiti kwenye mambo yahusiayo UFO na ambaye moja ya kazi zake ni ile inayo patikana kwenye filamu maarufu ya mwaka 1997, ‘Close Encounters of the Third Kind’ Mwaka 1969 Vallee aliandika kitabu chenye mvuto wa aina yake kwenye masuala hayo kilicho kwenda kwa jina la ‘Passport to Magonia’, Vallee anasema,
“…. Hadithi za kufikirika kwenye jamii mbalimbali duniani, imeonekana kuwa, zina kiasi kikubwa cha wapokeaji wa hadithi zinazo husu viumbe wanao karibiana na binadamu walio kuwa wakiruka angani na wakitumia vyombo na nyenzo  zilizo onekana ni bora kiteknolojia ukilinganisha na zama hizo.”( Jacques Vallee ‘Passport to Magonia’)
Watafiti wa UFO John Weldon na Zola Levitt ambao utafiti wao wameuweka kwenye kitabu walicho kiita, ‘What on Earth Is Happening?’ wanasema,

“UFO zinaonekana kuwepo kwa muda mrefu. Tunaweza kupata hadithi za kushangaza zinazo husu ‘maduara ya moto angani’ kwenye kumbukumbu nyingi za kihistoria na hata kwenye michoro ya mapangoni. Wakati tukijiona kuwa na taarifa nyingi zinazo husu UFO katika zama zetu, kila zama zinaonekana kuwa na hadithi kama hizi za kwetu (tunazo ripoti sasa kuhusu UFO)”( John Weldon na Zola Levitt, ‘What on Earth Is Happening?)
Kama tutazungumzia kuwepo kwa viumbe wengine ambao ni huru kama binadamu basi Misri ni nukta ambayo haiwezekani kuachwa kwenye mazungumzo hayo, hapa nitazungumzia kitu kingine kidogo tu kwenye mstari huohuo wa viumbe huru mbali na binadamu na mahusiano yake na vyombo visivyo fahamika kwenye anga la dunia.

Kwenye utamuduni wa kale wa kutoka Egypt na watu wake kumejaa visa vingi vinavyo wahusu ‘miungu wenye kupaa’ ambao walikuja duniani na kati ya mambo mengi ni kuwatawalia binadamu mambo yao na kuwaongoza. Vyombo walivyo tumia miungu hao ni ‘diski za duara’na ‘ngalawa zenye kupaa’ ambazo mwonekano wake ni sawa na maelezo ya watu wa zama zetu walio ona UFO.

Kutokana na hadithi za kale za watu wa Misri, mungu jua ambaye alifahamika kama Ra, alikuwa ndiye mungu wa ulimwengu wote na alikuwa akisafiri kwa kutumia‘ngalawa inayo paa’ Mungu huyu huoneshwa akiwa na mwili wa binadamu na kichwa cha ndege tai. Mungu mwana wa Ra aliitwa Horus, ambaye alizaliwa na mungu mama, bikira Isis. Mungu mwana huyu alikuwa ndiye mungu wa mbingu, mungu mwangaza na wema. Horus huoneshwa akiwa na umbile la binadamu na kichwa cha kipanga. Horus naye alisafiri angani akitumia diski yenye mbawa.( E. A. WALLIS BUDGE ‘THE BOOK OF THE DEAD’, The Papyrus of Ani).

  Isis mungu mama, bikira aliyemzaa mungu mwana Horus, wakati anatoroka kumuokoa mwanae ambaye ni Horus asiuwawe na Seth alisaidiwa na mungu Thoth kutoroka kwa kutumia boti yenye muundo wa disk inayo paa angani. Chombo alicho safiria angani mungu baba Ra, kilikuwa kiking’aa kwa rangi nyingi, maelezo ambayo yanafanana na chombo cha UFO.
Kuonekana kwa vyombo hivi vya ajabu Mashariki ya Kati viliendelea muda mrefu baada ya matukio kama hayo kwenye jamii ya watu wa Egypt wakale.
Katika kipindi cha dola ya wa Giriki na ile ya Roma kutoka karne ya nne BC mpaka kwenye karne ya 17 BC mara kadhaa vitu vya ajabu ambavyo muambilie na teknolojia yake ilikuwa hailingani hata kidogo na zama zenyewe vilionekana katika anga hizo.

Kutoka kwenye kazi ya Weldon Levitt kuhusiana na zama hizo na vyombo vya usafiri vya anga ambavyo havifahamiki wanasema,
 Maandishi ya mwana historia mmoja wa Kiroma, yamerekodi matukio ya vyombo visivyo fahamika kwenye anga la Roma kwenye karne ya tatu na nne BC. (http://www.hidden-science.net/EnglishBoard/viewtopic.php?f=12&t=248.)
  
Waandishi wa historia walio kuwa wakikubalika katika zama hizo kama Pliny, Seneca, Tacitus, na Lycosthenes wote wametaja kuhusu kuonekana kwa vyombo hivyo. Titus Livius na Julius Obdequens wame orodhesha sehemu nane tofauti ambazo vyombo hivyo vilionekana. (http://www.hidden-science.net/EnglishBoard/viewtopic.php?f=12&t=248.)



Zama zilizo fuata na karne zake ambazo zilishuhudia kunyanyuka na kuanguka kwa dola ya Roma, bado rekodi ya vyombo visivyo fahamika katika anga la sayari yetu iliendelea kuingizwa kwenye vitabu vya kihistoria duniani kote mpaka kwenye zama zetu hizi.
Nukta ambayo ingefuatia hapa baada ya hiyo historia fupi ni shuhuda rasmi kutoka katika serikali mbalimbali duniani na taasisi zake. Lakini huenda ni kutokana na muda au mchezo unao chezwa kuhusiana na suala hili binafsi sijaweza kupata ushuhuda huo, ingawa kupitia milango ya nyuma, vyanzo visivyo rasmi na wafanyakazi wa kiserikali kutoka eidha serikalini au taasisi na mashirika ya kiserikali yanayo husiana na masuala haya upo ushuhuda wa kutosha kwamba lisemwalo lipo.
Hivyo nukta hii nitaiacha ikining’inia kama haipo lakini nitakuwa nikiigusa moja kwa moja, au kupitia kwa katika mfululizo wa kazi yetu hii. Nitakuwa nikiigusa kwa namna ambayo baadhi ya serikali, taasisi na watendaji wao wanakiri waziwazi juu ya vyombo hivi na shughuli zake.

     Ikiwa UFO ni vyombo ambavyo havijulikani, na ikiwa vinaweza kufanya vitu vya ajabu na hatari kushinda hata vile ambavyo vyombo vyetu vya anga na vile vya kivita vinavyo weza kufanya, basi hapana shaka vyombo hivyo vinamilikiwa au vipo nyuma ya viumbe ambao ni huru. Swali la msingi ni; Je kuna viumbe huru katika sayari yetu na kutoka nje ya sayari yetu kama binadamu?

 Kwa ajili ya somo letu kuweza kueleweka vyema, na muhimu lieleweke vyema kwa sababu kama tulivyo ona kwenye posti hii(HATUA NNE KABLA YA UJIO WA MASIHDAJJAL/KRISTO WA UWONGO/MPINGA KRISTO/666) icheki hapa,http://salimmsangi.blogspot.com/2013/08/hatua-nne-kabla-ya-ujio-wa.html ni kuwa karata ya mwisho itakayo chezwa na maadui zetu kwa ajili waweze kututawala chini ya utawala wa kishetani ni kutuletea kitisho kutoka nje ya sayari yetu. Hivyo kati ya mengi hapa pia tutaangalia ikiwa kuna kiumbe kingine huru mbali na binaadamu, si kutoka kwenye sayari yetu tu, bali hata nje ya galaxy yetu ya Milk Way, Inshallah.

   

    Maoni ya wengi ni kuwa ‘viumbe kutoka nje ya sayari yetu’ na ambao wanatumia UFO ni wageni kutoka kwenye Galaxy nyingine mbali na hii ya kwetu. Viumbe hao husafiri mamilioni ya maili kwa muda mchache sana, kitu ambacho kinapingwa kutokana na ukweli kwamba kusafiri tu kutoka kwenye dunia yetu kuelekea kwenye nyota iliyo karibu sana na dunia yetu huenda ikachukua kwa uchache miaka 70,000. Kizingiti kikubwa kuhusiana na usafiri huu wa kutoka achilia mbali galaxy moja kwenda nyingine lakini kwenye nyota tu zilizo kwenye galaxy yetu ni nishati kiasi gani itahitajika kwenye safari kama hiyo ambayo mwendo kasi wake ni ule wa umeme. Kumbuka safari ya mwezini waliirekodi kwenye jangwa la Nevada na kudai ni mwezini. Nimeshalieleza hilo kwa kina kwenye posti hii, HATUKWENDA MWEZINI, unawweza kuipata hapa,http://salimmsangi.blogspot.com/2014/12/hatukwenda-mwezini.html


 Lakini huenda ‘ viumbe’ wanao endesha UFO wanayo teknolojia hiyo ya maajabu.
Lakini kuna shortcutsWormholes.


    
Kabla hatujaanza kuitizama ‘shortcuts’ kuna misamiati mitatu ambayo inabidi tuitizame na tuielewe kabla ya kuzama kwenye somo letu. Misamiati hiyo ni
Wormhole,
Timerelativity, na
 Blackhole.
Blackhole ni hali inayo tokea au ni mazingira yanayo patikana baada ya kifo cha nyota angani. Nyota hiyo ambayo utakuta ukubwa wake unazidi nyota yetu ya jua mara tatu mpaka  kumi na zaidi.  Nyota hiyo inapoishiwa na ‘mafuta’ yake inaongezeka ukubwa. Joto lake ambalo lilikuwa ni nyuzi milioni 15, linaongezeka na kufikia nyuzi milioni 100. Nyota hiyo hubadilika na kuwa nyota kubwa na nyekundu, ukubwa wake unazidi ukubwa wa nyota yetu ya jua mara milioni 60. (ametakasika Mola wangu Mbora wa Uumbaji)  Kutokana na kuwa nyota hii imeishiwa na mafuta yake inakuwa haina nguvu ya kuzishinda nguvu zake za mvutano na hivyo inajimeza yenyewe, inanyonywa na nguvu zake za mvutano na kutengeneza Blackhole.

     Tukio hili muhimu kwenye maisha ya nyota katika ulimwengu wetu limeelezewa katika Quran 56:75-76;
     “Basi naapa kwa maanguko ya nyota,”
“Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngelijua!”
     Blackhole unahusiana vipi na mada yetu hii? Kifizikia inafahamika kuwa hakuna chenye kukatisha Blackhole hata mwanga wenye kusafiri kwa kasi ya kilometa 300,000 kwa sekunde haukatizi kwenye shimo hilo! Lakini nadharia mbayo haijathibitishwa kabisa ni kuwa Blackhole inayo upande wa pili ambapo ni Whitehole. Utakapo zama kwenye blackhole utaunganishwa kupitia ‘Wormhole’ kufika kwenye Whitehole ambapo hapo utakuwa umetokea kwenye ulimwengu mwingine. Lakini nadharia hii haikamiliki mpaka kweli kuwepo na Whitehole mwisho wa blackhole na kuwepo na Wormhole ambavyo hivi vyote vipo kwenye nadharia.


     Kutokana na itikadi kwamba huenda kukawa na viumbe wengine ima katika galaxy au sayari nyingine walio piga hatua na maendeleo makubwa kiteknolojia na kiustaarabu kutushinda sisi, huenda hivi ambavyo katika ulimwengu wetu ni nadharia kwao vikawa ni maarifa yanayo fanyika kivitendo na vyenye ukweli wa msingi, hivyo kwa wao kutumia, blackhole, Whitehole, Wormholes ni kitu kinacho wezekana kabisa. Lakini swali ni je viumbe hao wapo? Kwa ushahidi upi tutatambua kama wapo?
     Wormhole kama tulivyoona  nayo ni tobo la kufikirika ambalo linasemwa linaweza kuunganisha sehemu mbili tofauti kwenye galaxy mbili tofauti, sayari au nyota na muda.
Safari kuelekea kwenye nyota nyingine au galaxy kupitia Wormhole inakuwa fupi sana. Lakini kwa sharti ya kuwepo kwa hiyo Wormhole. Katika ulimwengu wa dunia yetu hii ya tatu kutoka kwenye mfumo wetu wa jua, Wormhole bado ni nadharia piwa, hatujui kwa ‘hao’ wanao tajwa kuwa ni viumbe kutoka ulimwengu mwingine labda kwao ni ukweli wa msingi na wanaweza kusafiri kutoka kona moja ya galaxy, nyota au sayari kwenda nyingine kwa kutumia Wormholes. Lakini swali letu linabaki palepale, viumbe hao wapo? Ushahidi ni upi kuwa wapo?

     Hivyo kupitia kwenye Wormhole, sehemu mbili za ulimwengu tofauti yaani galaxy au nyota zinaweza kufikiwa, lakini zaidi pia muda tofauti na kwenye nukta ambayo safari imeanzia. Kabla ilikuwa ikichukuliwa kuwa muda upo sawa sehemu zote kwenye Milkway na kwenye galaxy nyingine. Lakini baadaye ikaja kuthibitika kuwa muda unatofautiana sehemu mbalimbali kwenye galaxy, sayari na nyota zingine, na hapa ndipo ugunduzi mkubwa wa watu kama Einstein, Galileo, na Aristotle ulipo kuja na theory of relativity’ autime relativity theory’.
 Ingawa wanasayansi na wanafizikia hawa nadharia hii imebaki bado ni nadharia, kwenye kitabu kitakatifu cha Quran mahali pengi time relativity’ haikutajwa kama nadharia bali; ukweli wa msingi. Tizama  Quran 70: 4, Quran 32: 5, Quran 10: 45, Quran 23: 112-113.
Kabla ya kulitizama hili la time relativity kwa mustakabali wa mada yetu, kwanza tujiulize  swali moja tata kidogo;
Wakati, muda, saa ni nini? AuWhat is Time?

Kama unatembea barabarani halafu mtu akakusimamisha, akakuomba samahani halafu akakuliza what is time? Hapana shaka utanyanyua mkono wako utatizama mashine iliyoko mkononi mwako au utalitizama jua na kisha utamuambia ni saa kadha, na dakika kadha halafu kila mtu ataendelea na ustaarabu wake.
Kiasi fulani hichi ndicho tunacho kijua kuhusiana na saa. ‘Muda hautoshi bana, tutaonana kesho.’Utawasikia watu wakisema, kila mtu anatamani lau tungelikuwa na muda zaidi, kila siku, muda, saa, wakati hautoshi, lakini what is time?
     Kuna leo, kesho na jana. Je muda ndiyo kizingiti kwamba hatuwezi kwenda kuiona kesho, kurudi kuioyana jana? What is time? Je tunaweza kurudi nyuma kwenda kumuona Yesu (Rehma na Amani ziwe juu yake) alivyo kuwa anahubiri na alikuwa akihubiri kitu gani? Je tunaweza kurudi nyuma na kwenda mwona Muhammadi (Rehma na Amani Ziwe Juu yake) na masahaba zake (Radhi za Mola wetu ziwe juu yao) katika moja ya vikao vyao? Lakini what is time? Ndiyo inayo tuzuia tushindwe kumuona Hitler? Ndiyo inayo tuzuia tusiende mwaka 2090 na kujua dunia itakuwaje?What is time? Kuweza kurudi nyuma kwenda kuiona ‘jana’ au kwenda mbele na kuweza kuiona ‘kesho’ wanasayansi wa leo katika fani husika wameiita hiyo hali nitime traveling’.

     Eidha time traveling inawezekana ama la lakini kwanzawhat is time? Inavyofahamika kisayansi saa ipo kwenye mstari ulionyooka, yaani ina mwanzo, kati na mwisho. Lakini relativity theoryinatupa mtazamo mwingine juu ya saa. Kwamba hali inayo itwa saa si kitu unacho weza kukishika, saa imeongezwa kwenye ulimwengu wetu wa 3D, na kuifanya kuwa ni 4D kwa dharura na kwenye mazingira fulani ingawa kiuhalisia na kimantiki hasa ulimwengu wetu  ni 3D. Saa kwa mtazamo wa sayansi ya kifizikia na kifalsafa ndiyo hali inayo tufunga tushindwe kusafiri kwenda kuiona kesho na kurudi nyuma kuiona jana.
     Kwa vile kimaumbile kitendo kilicho kwisha pita hata ndani ya sekunde iliyogawanywa hakiwezekani kamwe kubadilishwa, sekunde (saa) imeshapita, hatuwezi kimaumbile kurudi nyuma kabla ya tukio kufanyika na kuzuia lisifanyike au kulirekebisha namna ambayo linapasa kufanyika.

     Kama kilivyo kitu chochote ambacho kimerikodiwa iwe ni Quran katika CD, filamu au chochote kile, hata posti hii unayo soma, utaona kina mwanzo, kati na mwisho lakini kiasilia ni kitu ambacho kinapatikana katika hali ya ukamilifu wake, mathalani unaposikiliza CD hiyo kutakuwa na mwanzo, kati na mwisho wa kile ambacho unasikiliza au kutizama lakini kitu chenyewe kilivyo hifadhiwa kwenye chombo hicho hakina mgawanyo huo, bali mgawanyo wa eidha upo mwanzo au mwisho unategemewa na muda ambao muhusika anasikiliza/tizama kitu hicho. Ndivyo ulivyo wakati/saa, haina mwanzo wala mwisho bali sisi wahusika ndiyo tunaipa hali hiyo au aina hiyo ya mtazamo.

Na maanisha wewe hapo ulipo unapo soma posti hii, maisha yako na vyote vinavyo kuzunguka, na vitakavyo kuja au utakavyo fanya baada ya kumaliza kusoma hapa unapo soma ni kama kitu kilicho hifadhiwa kwenye CD, wewe unaona maisha yako yana mwanzo, yana kati na yatakuwa na mwisho, lakini kuna ambaye anayatizama maisha yako bila kuathiriwa na kitu ambacho wewe unakiita wakati/ muda/ saa, yeye anayaona hayo maisha yako yaliyopita, ya sasa na yanayo kuja kwa pamoja bila kuwa na mwanzo wala kati wala mwisho. Hii ni sifa ya MUNGU MMOJA ALIYETUKUKA, uonaji wake yeye hauathiriwi na muda.

 Ingawa kwenye kalenda yako wewe inasoma umezaliwa miaka 20, 30 au 40 iliyo pita, lakini machoni pa Mungu Mmoja wa Haki, tendo la wewe kuzaliwa linaonekana kama ndiyo unazaliwa sasa, ingawa utakufa miaka 20, 5, au 1 baadaye lakini machoni pa Mungu Mmoja wa Haki tendo la wewe unakufa linatokea au linaoneka hivi sasa. Hakuna mwanazo wala mwishoni machoni pa Mungu, hali zote, vitendo vyote, vinaoneka kwa wakati mmoja. Maumbile yetu hayaturuhusu sisi kuona hali katika sifa hiyo.

Ukiwa na mantiki hiyo kichwani mwako, kwamba wakati hauko kwenye hali ya mstari mmoja, hivyo hauna mwanzo wala mwisho bali ni hali itakayo pewa mtazamo huo na wahusika tofauti, mahala tofauti na mazingira tofauti, hapa ndipo inapo kuja nadharia nyingine kuhusiana na UFO. Kwamba je UFO na viumbe wanao endesha wanatokea katika wakati ujao.
     Nadharia hiyo inadai kuwa UFO watakuwa ni binadamu wa zama zijazo ambao teknolojia yao imekuwa ya hali ya juu kiasi kwamba wameweza kusafiri kutoka kwenye hali tunayo ita ‘wakati ujao’ na kuja kwenye ‘wakati uliopita’ ambao kwa wao ‘wakati uliopita’ ni ‘wakati uliopo’ kwetu sisi. Hivyo ni binadamu wanao toka katika wakati ujao, au pia inawezekana kuwa ni viumbe wanao toka kwenye ulimwengu mwingine ambao maendeleo yao ya teknolojia yana wawezesha kusafiri kutoka kwenye ‘wakati ujao’ na kuja kwenye ‘wakati ulio pita’ ambao kwetu sisi ni wakati uliopo kwa vile kitu unacho kiita ‘saa’ hakina mwanzo, kati wala mwisho na hakipo kwenye mstari ulio nyooka.

     Lakini kama watakuwa ni binadamu ambao maarifa yao yame wafikisha hapo na kuweza kufanya ‘time traveling’ yaani kutoka kwenye ‘hali’ moja ya ‘saa’ kwenda nyingine, haikubaliki kwa vile ‘mashuhuda’ wa vyombo hivyo na wale walio wahi ‘kutekwa’ na viumbe hao wanasema siyo binadamu!
Lakini juu ya yote ‘time traveling’ kwa binadamu haliwezi kufanyika KIMWILI bali KIROHO, kila mmoja wetu kwa nyakati tofauti amefanya ‘time traveling’ kiroho, yaani bila kiwiliwili, na hapo ni wakati unapokuwa NDOTONI, ambapo ‘unaota’ tukio ambalo linakuja ‘kutokea’ sehemu fulani kwenye nukta ya maisha yako.
Lakini kimwili inakuwa ni vigumu mno na sina muda wa kutosha kukuelezea kwa nini inakuwa vigumu, unless kama mada hiyo ikija kwa mfumo wa swali.
Lakini kama itakuwa ni viumbe wengine kutoka nje ya ulimwengu huu kama inavyo semwa basi, ushahidi wenye mashiko na misingi inayo eleweka na kukubalika lazima uwekwe mezani kuthibitisha kuwepo kwa viumbe hao, kitu ambacho mpaka sasa bado hakijafanyika.
Tumetoka nje kidogo na somo letu la UFO, ila nukta nilizo zitaja hapo juu tutakuwa tukizirudia mara kwa mara kutoka hapa na kuendelea.



Kitendo kinacho fanywa na UFO au tabia za UFO ambapo huweza kujitokeza na kupotea kwa kipindi cha kupepesa jicho tu, kusafiri kwa mwendo kasi mkubwa na kupinduka chini juu na juu chini au kugeuka katika nukta mbayo vyombo vyetu haviwezi zimechukuliwa kuwa ni tabia za ‘hyperdimensional’ au tabia kutoka kwenye galaxy nyingine.
Maumbile yetu au tabia zetu sisi binamu tunaweza kuutambua au kuuona ulimwengu wetu na vile vyote vinavyo tuzunguka kwenye mfumo wa ‘three dimensional’ (3D) yaani, urefu, upana na kimo. Chochote chenye zaidi ya 3D hatuwezi kukiona.  Mazingira ambayo kuna zaidi ya 3D yanafahamika kama ‘hyperspace’ au ‘hyperdimensional’. Ni vigumu mno na ngumu sana kwa mtu wa kawaida kuweza kuingiza kwenye akili yake na ‘kupiga picha’ kwenye ubongo ya namna ulimwengu wenye zaidi ya 3D unavyo onekana.
Mathalani tunapo zungumzia ‘two dimensional’ (2D) tunakuwa na ‘upana’ na ‘urefu’ tu. Tuashumu kuna ulimwengu wa kufikirika  wa 2D ambapo kuna viumbe wanaishi kwenye ulimwengu huo. Ni wazi kuwa kile ambacho wanaweza kuona na kuhusu viumbe hawa ni kile tu ambacho kitakuwa kwenye 2D. Tuashumu kinakuja kiumbe kutoka kwenye ulimwengu wa 3D na hapo kiumbe hichi kinachomeka kidole chake kwenye ulimwengu wa 2D. Kile ambacho viumbe wa ulimwengu wa 2D watakacho ona si kidole bali duara, kwani uwezo wao wa kutambua kitu umesimamia kwenye ‘urefu’ na ‘upana’ hamna ‘kimo’ .Duara hilo (kidole) hicho kitaonekana kuwa kimetokea ghafla kusiko julikana na pia kupotelea kusiko julikana. Lakini ni kuwa mwenye kidole hicho anaweza kuwatisha na kuwasumbua wa kazi wa 2D kwa vile tu yeye ana 3D. Anaweza kukitoa hapo na kukipeleka sehemu nyingine yoyote apendayo katika ulimwengu wa 2D kwa tabia na sifa ambazo kwenye ulimwengu huo ni kitu ambacho hakiwezekani.

Tunapolitazama suala la UFO leo hii ambapo mfumo wa mawasiliano na vyombo vya habari umewafungua kwa kiasi fulani walimwengu kuhusiana na elimu ya anga na uwezekano wa kuwepo viumbe wengine nje ya dunia yetu, katika ulimwengu wa leo ambao  mambo ya ‘New Age’ na imani yake inakaribia kuchukua nafasi ya imani za kidini kwa baadhi ya dini na madhehebu, suala la UFO nalo lina waumini wake wanaolikubali kiimani zaidi kuliko . Hivyo kuliachia suala la UFO kwenye ulingo wa teknolojia peke yake bado hatutakuwa tumelitendea haki.

Tukiacha upande wa sayansi na tekinolojia au ‘bati na nondo’, UFO kwa baadhi ya wachambuzi ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko uhalisia wa kitu chenyewe.  Wachambuzi hao wana simamia kuwa suala la UFO ni hitajio la kisaikolojia ambalo limetengenezwa na maono ya mtu binafsi au imani yake na kutimilizwa na ubongo wake. Ubongo kama ulivyo na ufanyaji kazi yake ni fumbo ambalo utatuzi wake bado umbali sana kutatuliwa. Kile ambacho tunacho kifahamu kuhusiana na ubongo, hasa kwa kutegemea kile ambacho tuna pata kupitia mitaala iliyopo kwenye ngazi mbalimbali zilizopo katika mfumo wetu wa elimu ni kidogo sana. 
Ubongo si mada kuu hapa hivyo nachilia kukutwika maelezo ambayo yatakutoa nje ya somo letu, hivyo kwa wakati wako binafsi kajifunze hilo, isipokuwa  ubongo unaweza kukuletea au kukutengeneza umbo la kitu au kiumbe kilichopo kwenye 3D na kikasimama mbele yako. Mathalani nimepata kusoma maandishi ya mtu mmoja aliye dai kuwa yeye binafsi amekwenda  ‘mbinguni’ na kukanyaga aridhi yake  aliyo sema ni dhahabu tupu na waka shikana mikono na Yesu. Lakini pia nimepata kusikia mfano wa hayo kutoka kwa watu mbalimbali. Leo kwenye fukuto la ’New Age’ hadithi kama hizo zinajaza maelfu ya vitabu, lakini je, zina beba ukweli wowote wa msingi?
Jibu ni hapana.


     Lakini kuliweka sua la UFO kwenye uchambuzi wa kisaikolojia peke yake pia unashindikana kutokana na kwamba baadhi ya UFO zilizo pata rikodiwa kuna zile ambazo zilizo dondoka au dondoshwa na makombora na baadhi ya masalio yake kuokotwa kwa ajili ya uchambuzi na kumbukumbu.
Tunaweza kusema kuwa UFO na viumbe wanao vimiliki vyombo hivyo wanatokea katika Hyperdimensional. Lakini swali ni moja tu, je kuna viumbe wengine kwenye hiyo hyperdimensional, je wapo viumbe wengine katika sayari za mbali, nyota au kwenye  galaxy?
    
Katika zama zetu hii leo ‘zama za sayansi na teknolojia’ na sakata la kuwepo kwa viumbe wengine huru ni suala ambalo limekuwa likielezewa zaidi na filamu za Hollywood kuliko kwenye maabara za sayansi hiyo. Ni suala ambalo limeandikwa sana kwenye hadithi za kufikirika kuliko vitabu rejea vya mashuleni. Ni suala ambalo halijathibitishwa rasmi katika maeneo  karibu yote ya hatua mbalimbali za mifumo mbalimbali ya elimu tuliyo nayo. Zaidi ya maelfu kama siyo mamilioni ya filamu na tamthilia kutoka maeneo mbalimbali ya dunia zinazo elezea juu ya kuwepo kwa viumbe hao, mamilioni ya nakala zikiwemo vitabu na makala zenye maudhui ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia juu ya kuwepo kwa viumbe hao, hakuna ukweli wa msingi uliothibitishwa rasmi na vyombo huru vinavyo tegemewa kwenye fani hiyo hasa ya elimu ya anga juu ya kuwepo kwa viumbe hao.


     Ni suala ambalo limemeza fikra na mitazamo ya watu hasa katika karne hii, na hivyo inaniwia vigumu binafsi kulipinga kwa aya moja tu hapo juu, lakini hata hivyo fikra na mitazamo hiyo juu ya kuwepo kwa viumbe hao huru kama binadamu haijasimamia kokote zaidi ya kwenye ulimwengu wa filamu, katuni, tamthilia na vitabu vyenye hadithi za kufikirika zaidi.

     Karibu kila filamu, tamthilia au kipindi cha luninga kinacho zungumzia kuhusu ujio wa viumbe kutoka nje ya sayari yetu, utakuta kiongozi wakazi hiyo ni Freemasons. Mathalani  Close Encounters of the Third Kind, ET, Taken, Alien 14, Independence Day, 2001: Space Odyssey, Star Wars, Star Trek, Men In Black, From the Earth to the Moon, Apollo 13, War of the Worlds, na XFiles.
Gene Roddenberry, mtengenezaji wa Star Trek alikuwa ni Freemasons wa daraja la 33. Hii ndiyo sababu ya kuwepo kwa alama nyingi za kimasoni kwenye filamu hiyo. George Lucas. mtengenezaji wa Star War naye alimimina alama na nembo nyingi za kimasoni kwenye kazi yake hiyo.


Alama hizo za kishetani na kimasoni kwenye kazi zao mbalimbali zinazo patikana katika ulimwengu wa burudani, zinaeleweka vyema kwa wafuasi wa taasisi hizi za kishetani kuliko kwa watazamaji na wasikilizaji wa kawaida ambao kwa wao zinabaki kama fumbo lisilo na mtatuzi. Hata hivyo nembo na alama hizo zinalenga kabisa kupandikiza maudhui hayo ya kishetani na kimasoni katika hatua mbalimbali za maisha yetu na katika harakati mbalimbali za kila siku za maisha yetu. Zinalenga kutufanya tuwaze, kufikiri na kutenda kama wanavyo taka maadui zetu na watawala wao bila sisi wenyewe kufahamu.



Spielberg ambaye pia alikuwa ni mtengenezaji mkuu wa Men in Black II, filamu inayo zungumzia serikali ya siri ambayo kazi yake kubwa ni kuwalinda watu kutokana na kitisho cha viumbe kutoka nje ya dunia. Februari 1997 shirika la filamu Uingereza lilivujisha habari kwamba Spielberg na viongozi wenzake wa Dream Works kwa siri walikutana na viongozi  wa Pentagon ndani ya Los Angeles. Viongozi hao walimuambia ‘acha kila kitu’ na atengeneze filamu ambayo maudhui yake yatakuwa yanahusu vimondo.

Mwaka mmoja baadaye filamu ya Deep Impact ilitengenezwa. Filamu ambayo inazungumzia vimondo vinavyo anguka kwenye uso wa dunia yetu. Ni akina nani hao viongozi wa Pentagon na kwa nini walikuwa na hamu kubwa kwa Spielberg kutengeneza filamu inayo zungumzia kitisho kutoka nje ya dunia?
Spielberg amehudhuria mkutano wa asasi ya siri ya Bilderberg wa mwaka 1999 na mikutano mingine ya asasi hiyo. Disemba ya mwaka 2002, mtandao wa luninga wa SciFi ulionesha dokumentari, zilizomo kwenye utaratibu wa wa miniseriesya masaa 20, ambazo zililenga kuonesha uvamizi wa viumbe toka nje ya sayari yetu wakiwateka binadamu. Gharama za utengenezaji wa kazi hiyo ilifikia dola za Marekani Milioni 120 na kuifanya kuwa ni moja ya miniseries yenye gharama kubwa sana kupata kutengenezwa. Unaweza kudhani kuwa Spielberg kwa sasa amechoka na kutengeneza kazi za namna hii. Lakini mabwana wakubwa waliomshika akili yake kiukweli wanayo hamu kubwa sana ya kuona fikra hizi za kuwa kuna viumbe wengine nje ya sayari yetu (na ambao ni hatari mno na wanao weza kutuvamia na kutushambulia na kutusambaratisha kabisa tusipo ungana, kuwa fikra hizi zinaingia kwenye akili za watu na kuwa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku).


Kwa hivi sasa wale watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wao wakiwa ni vijana, na wale wenye matumizi ya kutumia barua pepe, na wale wanao shusha huduma mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya intaneti wataona kabla hawajafanya yoyote kati ya hayo kuna hatua ya kujisajili ambayo kwanza lazima uipitie, katika hatua hiyo kuna mahala ambapo utatakiwa kuingiza aina fulani ya herufi na tarakimu ambazo ziime changanywa na kutakiwa kuziingiza kwa usahihi. Unajua ni kwa nini unatakiwa kuingiza namba na tarakimu hizo? Kwa sababu wanataka kuhakikisha anayetaka kutumia huduma hiyo ni binaadamu. Nambari hizo na tarakimu kwa namna zilivyo andikwa zitatambuliwa na binadamu tu, hivyo ndivyo wanavyo sema. Sasa jiulize ni nani atakayetumia huduma hii ya kompyuta na intaneti zaidi ya binadamu? Wanadhibiti viumbe kutoka nje ya sayari yetu ambao inasemekana tayari wapo na wanaishi na sisi katika dunia yetu hii ya tatu kutoka kwenye jua ndani ya galaxy ya Milkway, wasitumie huduma hizi za mawasiliano kwa sababu mbalimbali. Lakini je ni kweli wapo?

Itaendelea Inshallah ....

Post a Comment

0 Comments