Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHAZ ya hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi
nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe mtu wanguvu uzione labda iko
itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini nd’o mjengo huo yani. Bubble House, iko Ufaransa.
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwa Shoe House, iko South Africa.
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena