Kampeni ya Zamu Yako 2015 inaendelea kuwahamasisha watu hasa vijana kupiga kura na kutambua umuhimu wa zoezi hilo linaloendelea kuchangiwa na wasanii wengi kuwahamasisha vijana kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kumchagua kiongozi bora.
Msanii ambaye hivi sasa anaendelea kufanya vyema baada ya kushirikiana na diva ambaye ana uwakilisha mkoa wa Mbeya mwanadada Ney Lee katika wimbo wake uitwao 'Kumbe ni ndugu' Real Jofu ameelezea huu ni wakati kwa vijana wenzake kuwa Tanzania inataka mabadiliko na inampasa kijana kufanya chaguo sahihi kwa kupiga kura.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena