Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini. Analaumiwa kusababisha machafuko yaliyotokea Afrika Kusini kutokana na kauli yake aliyoisema kwamba wageni wanatakiwa warudi kwao. Jumatatu April 22 amekanusha kushinikiza machafuko hayo
Mitandaoni kumekuwa na picha na video nyingi zimesambaa zikionesha hali ilivyokuwa Afrika Kusini kwa zaidi ya wiki moja, tumesikia na kuona mashambulizi ambayo wamefanyiwa watu ambao sio raia wa Afrika Kusini ndani ya nchi hiyo, video nyingi na picha zinasikitisha.. watoto wanauawa, wanajeruhiwa.. vurugu ilikuwa kubwa sana.
Hapa ni ndani ya Kambi ya muda ambayo wamehifadhiwa wageni, yani walikuwa na maisha yao kawaida tu mtaani baadae wanajikuta ni wakimbizi.
Cha mwisho kilichonifikia ni kuhusu ishu ya Waziri wa Usalama wa South Africa,Nosiviwe Mpisa-Nqkula kutangaza kwamba sasa wanaoingia kupambana na watu wanaofanya vurugu hizo ni wanajeshi baada ya kuonekana kama Polisi wameelemewa nguvu na hali ilivyo mitaani, watu saba waliripotiwa kufariki pia.
Mtaani hali haikuwa sawa, hili ni sehemu ya kundi kubwa la watu waliokuwa wanaandamana kupinga Xenophobia, ubaguzi wa kutaka wageni waondoke Afrika Kusini.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena