Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA AFANYA MATEMBEZI MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA MOBISOL.

Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslaus Mabula akipokea Moja ya aina ya Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Jua ambao uliahidiwa kutolewa na Kampuni ya Uuzaji wa Mitambo ya Kufua Umeme wa Jua ya MOBISOL kwa ajili ya kupelekwa katika maeneo yenye uhitaji wa Umeme kama vile Vituo vya Zahanati Jijini Mwanza. 

Hii ilikuwa jana Wakati
Mstahiki Meya Mabula alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo ya MOBISOL Kanda ya Ziwa yaliyopo Kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza. Wengine katika picha ni Albert Msengezi (Kulia) ambae ni Meneja Masoko Mobisol Kanda ya Ziwa pamoja na Harry Oning'o (Kushoto) ambae ni Afisa Masoko Mobisol Kanda ya Ziwa.
Na:George GB Pazzo
Kutoka Kushoto ni Afisa Masoko Mobisol Kanda ya Ziwa Harry Oning'o akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Katikati) pamoja na Meneja Masoko Kampuni ya Mobisol Kanda ya Ziwa Albert Msengezi (Kulia).
Afisa Masoko Mobisol Kanda ya Ziwa Harry Oning'o (Kulia) akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Kushoto).
Meneja Masoko wa Kampuni ya Uuzaji Mitambo ya Kufua Umeme wa Jua (Solar) ya MOBISOL Albert Msengezi (Kulia) akitoa ufafanuzi wa Mitambo inayouzwa na Kukopeshwa na Kampuni ya Mobsol kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa pili kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Kisesa siku ya jana.
Ukisoma Ukutani utaona aina ya Solar zinazouzwa na hata kukopeshwa kwa Wateja wa Mobisol ambapo Kuna Solar ndogo iliyopewa jina la Chui inayozalisha Watts 30 kwa ajili ya Mahitaji ya taa na redio ndogo.
kuna Solar inayozalisha Watts 80 iliyopewa jina la Nyati kwa ajili ya Matumizi ya Taa, Radio na Tv, lakini pia kuna Kiboko inayozalisha Watts 120, na Kuna Tembo ambayo inazalisha Watts 200 ambapo zote hizo zinazalisha Umeme kwa ajili ya Matumizi ya Taa, Radio, Tv pamoja na Matumizi mengineyo. 
Mnunuzi anaweza kujioatia Solar hizo kwa kulipa pesa taslimu au anaweza Kukopeshwa na akawa analipa kidogo kidogo hadi Miaka Mitatu.
Kushoto ni Samwel Schuster ambae ni Meneja Miradi Kanda ya Ziwa kutoka Kampuni ya Mobisol akimlaki Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Kulia) ambapo katikati ni Albert Msengezi ambae ni Meneja Masoko Kanda ya Ziwa kutoka Kampuni ya Mobisol.
Katika Mahojiano ni GB Pazzo (Kulia) na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (Kushoto) ambapo aliipongeza Kampuni ya Mobisol kwa huduma zake nzuri na za uhakika zinazotolewa kwa wananchi.
Zaidi aliishukuru pia Kampuni ya Mobisol kwa kuahidi kusaidia Mitambo ya Kufua Umeme (Solar za Mobsol) katika maeneo yenye uhitaji wa Umeme kama vile Vutuo vya Afya na Zahanati Jijini Mwanza. ZAIDI BONYEZA HAPA
Credit:Radio Metro

Post a Comment

0 Comments