2015 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania,
 kila siku stori za Siasa zimekuwa kwenye headlines nyingi kuanzia 
Magazetini, kwenye TV, Radio na hata mitandaoni.
Mbunge James Lembeli
 alikuwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na 
Maliasili.. kuna stori za baadhi ya Wabunge wametangazwa kuhama Vyama 
vyao, Lembeli kathibitisha kuhama CCM kwa maneno yake mwenyewe.
>>> ‘Nimetafakari,
 nimezungumza na mama yangu kwa zaidi ya saa kumi.. mke wangu na watoto 
wangu, na kwa kusikia kilio cha wananchi wa Jimbo la zamani la Kahama 
nimeamua kutangaza kuanzia leo kwamba natangaza kujiondoa uanachama 
wangu ndani ya CCM‘ >>> James Lembeli.
>>>’Nilikipenda
 lakini nimelazimika kuchukua uamuzi huu, najua nawakera wengi lakini 
nawaomba waangalie hali ambayo Viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama 
wamesababisha niamue uamuzi huu mgumu‘>>>
>>> ‘Kuanzia
 leo najiunga na CHADEMA… Namshukuru Rais Kikwete, nafikiri atakuwa mtu 
wa kwanza kuamini haya ninayosema, mwaka 2010 mizengwe iliyofanyika 
lengo lake ilikuwa kukata jina langu, kila mtu anafahamu Rais mwenyewe 
aliwahi kuniambia lakini Rais Kikwete ndiye aliyerudisha jina langu… 
Ninaahidi nitaendelea kufanya kazi nae mahali popote, na MUNGU naomba 
anisaidie niweze kuvuka salama katika haya‘>>>> James Lembeli.

0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena