Nimekutana na stori mmoja kutoka Ufaransa inayomhusu mtoto wa miaka 18 aliyeweza kuishi na Ukimwi kwa miaka 12 bila kutumia dawa zozote wala vidonge vyovyote vya ARV.
Kitendo hiki kimeweka headlines nyingi sana nchini Ufaransa na kimeleta matumaini mapya ya kupata tiba ya ugonjwa wa Ukimwi, kwa njia ya kushusha virusi kwa viwango vya chini mwilini bila kutumia tiba ya kupunguza makali.
Na tangu
kipindi hicho ameweza kuishi na virusi hivyo bila venyewe kuonekana
kwenye damu yake na bila kutumia dawa yoyote hali inayojulikana kama “remission” – virusi kutokuongezeka wala kupungua mwilini, kwa miaka 12.
Madaktari
wanaamini kutakuwa na kitu cha tofauti kwenye mfumo wake wa damu
iliyoiwezesha dawa alizokuwa anazitumia akiwa mtoto kudhibiti ongezeko
la virusi, lakini kwa sasa hali nzima juu ya uvumbuzi huu bado ni utata
kwa madaktari.
Daktari kutoka The Institut Pasteur nchini Ufaransa amesema
kwamba hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka mingi kwa hali hii
kujitokeza kwa watoto ama kijana kwenye ripoti aliyowasilisha kwenye Press Conference ya The 8th IAS Conference on HIV Pathogenisis Treatment and Prevention mjini Vancouver wiki hii
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena