









Mwigulu Nchema ambaye ni Mbunge wa Sita
tangu Wilaya ya Iramba ianzishwe,amepokea Kijiti cha Ubunge Mwaka 2010
kutoka kwa Aliyekuwa Mbunge Ndugu.Kirimba.Mara baada ya kuchukua Ubunge
wa Iramba ,Mwigulu Nchemba amebadilisha sura ya maendeleo ya Jimbo hilo
katika maeneo ya Fuatayo.
Mwigulu Nchemba wakati akiingia kuwa
Mbunge wa Iramba alikuta Wilaya inaumeme maeneo ya Tarafa tu,Kata na
Vijiji vilikuwa havina Umeme.Hivi sasa Mwigulu Nchemba amefanikiwa
kuwasha umeme katika kata zote na Vijiji 48 vya Jimbo Zima.Hii haikuwahi
fanyika kabla ya Mwigulu kuwa Mbunge wa Iramba.
Mbali na Umeme,Mwigulu Nchemba akitambua
shida ya Maji inayolikumba jimbo lake,Amefanikiwa kufungua miradi 8 ya
Maji katika Kata ya Ndago,Shelui,Mgongo,Kyengege,KInapanda n.k Wakati
huo vijiji Zaidi ya 62 hivi sasa visima vinachimbwa ilikufanikisha
huduma kwa Wananchi wake.Pia ujenzi wa barabara za ndani ya Jimbo na
hata za kuunganisha na wilaya zingine zimeimarishwa na hata kupandishwa
daraja kuwa chini ya TANROADS.
Kwa maendeleo hayo na mengine kama
Kusomesha watoto wa familia zisizojiweza Zaidi ya 200,Kusambaza vitabu
kwa kila shule vyenye thamani ya Tsh.Milion 7 kwa kila shule.Pia
amekwenda mbali zaidi amekuwa Mbunge wa Kwanza kusambaza dawati 200 kwa
kila shule ya Jimbo lake na Mbunge pekee aliyechangia Mifuko zaidi ya
100 kwa kila shule kwaajili ya Ujenzi wa maabara pamoja na Flame zake za
Madirisha na Milango.
Maendeleo yote haya ambayo hayakuwahi
kufanywa na wabunge waliopita kunampatia nafasi kubwa sana Mwigulu
Nchemba kuendelea kuwatumikia wananchi wa Iramba,Kwa Taasisi za Kidini
amekuwa mstari wa mbele kujenda na Kufunika Makanisa na Misikiti
mbalimbali ndani ya Jimbo lake.
Wananchi wa Iramba hii leo wamejumuika naye kuhakikisha anakamilisha hatua zote za ndani ya Chama na taratibu za Uchaguzi ili tar.25/10/2015 aweze kuchaguliwa tena kuwaongoza.
Wananchi wa Iramba hii leo wamejumuika naye kuhakikisha anakamilisha hatua zote za ndani ya Chama na taratibu za Uchaguzi ili tar.25/10/2015 aweze kuchaguliwa tena kuwaongoza.
Mwigulu Nchemba anaandika historia ya
pekee kuwa Mbunge wa Iramba mwaka 2010,Mwaka 2011 analiteuliwa na
Mwenyekiti wa CCM Mh;Jakaya Mrisho kikwete kuwa Mtunza hazina ya CCM
Taifa,Mwaka 2012 Mwigulu anachaguliwa tena kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Tanzania Bara ikiwa ndio mara ya kwanza CCM inakuwa na Kiongozi
Mkubwa(Top 4) mwenye Umri chini ya miaka 40.
Mwaka 2013 Mwigulu Nchemba ameteuliwa
kuwa Naibu Waziri wa Fedha anayehudumia Sera.Mtiririko huu wa Uongozi
na kwa kuzingatia namna alivyokuwa mstari wa mbele kusimamia maslahi ya
Watanzania wote (wanyonge na Masikini) na hatiye kujitosa kuwania Urais
wa Jamhuri ya Muungano.Mwigulu Nchemba anaonekana ni TAA mbele ya
Wanairamba na hivyo wamekuwa wakisisitiza kuwa ndiye chaguo lao na
Wanaimani naye kubwa kuwa atawasadia katika kupandisha shughuli za
maendeleo yao.
Kauli mbiu ya Mwigulu iliyoshika kasi Nchini kwa sasa ni "MABADILIKO NI VITENDO NA WAKATI WAKE NI SASA"
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena