MADIWANI
wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara wamevunja baraza la Madiwani huku
wakiishinikiza Serikali kuwaeleza hatma ya pesa zao za pensheni tangu
walipoingia kwenye nyazifa hiyo mwaka 2015.
Diwani
Peter Ayoyi (CCM) wa Kata ya Mirare Wilayani Rorya mkoani Mara akitoa hoja zake
wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Rorya
|
Diwani wa Kata ya Mirare Piter Ayoyi (ccm) alihojikuwa ni kwanini Fedha kwa Madiwani haziko wazi wala haijulikani muda wa kulipwa licha yakuwa kwa upande wa wabunge Serikali imesema wazi muda na kiasi cha fedha watakazolipwa .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Roche Charles Ochele(ccm) alisema kuwa swali hilo ni gumu kujibiwa na Halmashauri kwakuwa wahusika ni Serikali kuu ambao ndiyo watakaoshughulika na fedha zao nakwamba hawajasema kiasi na nilini Madiwani watalipwa pesa zao.
Diwani wa Viti maalumu Pendo Odelle(ccm) alisema kuwa ni vyema Serikali kuu ikahalakisha fedha zao kama walivyoeleza wazi kwa wabunge kwakuwa fedha hizo walizitegemea ziwasaidie kwenye Kampeni zao katika uchanguzi.
“Serikali iharakishe fedha zetu,katika vikao vya kawaida vya Baraza la Madiwani tulikuwa tukilipwa posho za vikao kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri kati ya laki moja na nusu hadi laki moja na themanini”alisema Odele.
Anaongeza”Posho za mwezi Madiwani tulianza na laki moja na nusu baadae zikaongezeka hadi laki mbili na nusu na kisha laki tatu nanusu, kwahiyo kihalali Serikali inatakiwa itulipe pensheni milioni 21 yaani laki tatu na nusu mara miezi kumi na mbili mara miaka mitano lakini tetesi nikwamba tutalipwa kati ya milioni 9-10”alisema
Waamai
wanaotembeza madawa ya miti shamba Mjini Tarime mkoani Mara wamepata
wakati mgumu kuandikishwa kwa ajili ya kupata vitambulisho baada ya
kudaiwa kutotambuliwa na wenyeviti wa mitaa kutokana na kutokuwa na
makazi wala kutofahamika mitaa wanakoishi.
Wakiwa wamejipanga kwenye mistari kungoja kujiandikisha kwenye kituo cha uandikishaji wa vitambulisho mtaa wa Mwangaza Kata ya Nyamisangura mjini Tarime Mwenyekiti wa Mtaa Abdalla Mauridi aliwahoji wamasai watatu kuwa wanaishi ubarozi wa nani na kama wamepanga wamepanga kwa nani ambapo walisema hawana makazi maalumu.

Vijana wa jamii ya maasai-picha ya mtandao
...............................................
Musa
Oneremit alisema kuwa wao ni wazaliwa wa Ngorongoro –Arusha wako
Tarime tangu januari wakijishughulisha na biashara ya kutembeza mitaani
dawa za mitishamba na kwamba wao uzungusha biashara na ifikapo usiku
ulala kwenye gest mbalimbali mjini humo.
“Sisi tunatembeza dawa tumekuja Tarime tangu mwezi wa kwanza tunaweza kukaa hadi miezi sita kisha tunarudi Ngorongoro kutafuta dawa tunapokuwa hapa tunatembeza madawa kwa watu usiku ukifika tunalala kwenye Gesti sisi ni watanzania tunaomba tupate vitambulisho kura tutapigia hapa Tarime”alisema Oneremit.
Lebahati Olekambusi alisema iwapo watakosa fursa ya kuandikishwa kupewa kitambulisho ni kutowanyima haki yao ya kupiga kura,Pamoja na Maelezo yao Mwenyekiti Mauridi aliwakatalia kujiandikisha na kuwataka wamasai hao waende uongozi wa juu kwa mtendaji wa kata au kwa Mkurugenzi wa Halmashauri wakajieleze watakavyosaidiwa kwakuwa si wakazi wa mtaa wake.
Mwananchi ikiwa kwenye kituo hicho cha kupigia kula na kushuhudia kinachoendelea ililazimika kumtafuta kwa simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Venus Mwamengo na kueleza kilichojili kwa watu hao ambapo Mkurugenzi huyo alifika maramoja kwenye kituo kuwasikiliza.
Mwamengo aliwahoji kama wanavitambulisho vyovyote vinavyowatambua kuwa ni Raia wa Tanzania ambapo Musa Onekemit alitoa kitambulisho cha uanachama cha CCM huku wngine wakiwa hawana kitambulisho chochote,walikataliwa na hivyo kutakiwa kujaza fomu kwenda kwa Mkurugnzi ili wachunguzwe zaidi .
“Kuna wamasai wa Tanzania na wa Kenya ili tuthibitishe kuwa ni wazaliwa wa Ngorongoro ingieni kwa waandikishaji wa bvr mjaze fomu mzilete kwa Mkurugenzi sisi tunataraibu zetu tutafatilia huko ngorongoro kujua kama ni wazaliwa kisha mtapewa vitambulisho hata kama muda wa uandikishaji ukipita tukiwathibitisha nina kibari cha kuwapeni Vitamburisho”alisema Mwamengo.
Majibu hayo yaliwapa matumaini na kisha kujaza fomu ambazo zitashughulikiwa ndani ya siku mbili na baada ya kuthibitika kuwa ni wazaliwa wa Ngorongoro watajiandikisha na kupatiwa vitambulisho,na muda si punde wamasai wengine watano walijitokeza kwenye kituo hicho na kujaza fomu baada ya kupatiwa maelekezo.

0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena