Header Ads Widget

Responsive Advertisement

PICHA | JAJI MSTAAFU AMNADI KIJANA WAKE JIMBO LA KAWE

Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akizungumza wakati akiwanadi Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia) na Mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo, Charles William Iteba  katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akipongezwa na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia  mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akiagana na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia  mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kippi Warioba akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Kippi Warioba akibadilishana mawazo na Mmoja wa makada wa CCM waliohudhuria mkutano huo. Kulia ni Mkewe Nkaleni Warioba.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Zarina Madabida akiongozana na Kippi baada ya mkutano kumalizika.
Mtoto akiwa bango lenye picha ya Kippi Warioba.
----
Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, amesema anafahamu changamoto zinazowakabili wamachinga, mamalishe, baba lishe na wajaririamali wadogo; na kuomba wamchague ili azishughulikie.

Aidha, baba mzazi wa mgombea huyo, Jaji Joseph Warioba, amewataka wakazi wa Kawe wamchague kijana wake kwa kuwa ni msikivu, anayejituma na siyo mtu wa kusukumwa.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Songas ulipo Kata ya Makongo Juu juzi, Kippi alisema amewahi kufanyakazi na sekta binafsi ambayo ilimkutanisha na wajasiriamali, vikundi vya ujenzi, Saccos na Vicoba, hivyo alifanikiwa kujua changamoto zinazowakabili.

“Changamoto za makundi haya nazifahamu, nafahamu mnahitaji mafunzo na rasilimali mbalimbali kuendesha biashara zenu nithibitisheni Oktoba 25 nikazifanyie kazi,” alisema.

Kuhusu Makongo Juu, Kippi alisema Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, imeainisha kwamba barabara ya Makongo kuanzia Chuo cha Ardhi hadi Goba itajengwa kwa kiwango cha lami na tatizo la maji litakwisha kwa kuwa serikali itakamilisha mradi wa kutoa maji Kimbiji hadi Dar es Salaam.

“Matatizo ya michango mingi shuleni ambayo wazazi wanailalamikia, uhaba wa madawati, matundu ya vyoo, vitabu na madawati ni mambo ambayo tutashirikiana kwa pamoja kuyatatua wala hayahitaji mipango mikubwa ya serikali,” alisema.

Alisema wakazi wa Kawe wanapaswa kumchagua Dk. John Magufuli, yeye (Kippi) pamoja na madiwani wa CCM ili wakamsaidie kazi ya kutekeleza ilani.

Naye Jaji Warioba alisema wakazi wa Kawe hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani kwa kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Magufuli, itafanyakazi nzuri.

Alisema Dk. Magufuli ni mtendaji mzuri asiyependa rushwa hivyo ni wajibu wa wananchi kumchagulia wasaidizi kutoka CCM ili wakafanyekazi ya kuwatumikia.

Alisema hulka za Dk. Magufuli zinafanana na za mtoto wake (Kippi), kwa kuwa naye ni mchapakazi, msikivu na mtu mwenye ushirikiano mkubwa.

Naye mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo Juu, William Iteba, alisema kero za wakazi wa kata hiyo zinajulikana ikiwamo ukosefu wa kituo cha polisi, soko na ajira; hivyo akichaguliwa atatatua kero hizo
Dar es Salaam . Wakati kasi ya maambukizi mapya ya Ukimwi ikipungua nchini, tafiti zimebainisha Jiji la Dar es Salaam linashikilia nafasi ya sita miongoni mwa majiji yaliyoathirika zaidi barani Afrika. Takwimu hizo zipo kwenye ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) uliofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuangalia namna jamii za watu wa maeneo ya bandari walivyo na uwezekano wa kupata maambukizi mapya ya ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa mataifa mbalimbali. Mshauri wa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS), Marie Engel katika uwasilishwaji wa ripoti hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salam alisema ingawa maambukizi yamepungua nchini, bado Dar ni miongoni mwa majiji yaliyoathirika zaidi. “Dar es Salaam ni jiji la sita kati ya 10 yaliyoathirika zaidi Afrika ikiwa na asilimia 6.2 za maambukizi mapya kwa mwaka. Maambukizi ya ndani yamepungua kwa kiasi na mpaka mwaka jana yalikuwa asilimia tano maeneo ya mjini na 7.2 vijijini huku wastani kwa nchi nzima ukiwa asilimia tano,” alisema Marie. Alifafanua kwamba vita dhidi ya ugonjwa huo vinaendelea na kwamba jamii ya kimataifa inaamini mpaka mwaka 2030 utakuwa historia ingawa kuna kazi kubwa inahitaji kufanywa ili kufikia lengo hilo la kuukabili Ukimwi ulianza kuenea miaka ya 1980. MWANANCHI.

Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNICZ

Post a Comment

0 Comments