Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa
maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha.
Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane
za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya
Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi,
Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
Na
kwa sasa kamati maalumu ya kukusanya maoni ipo mkoani Tabora ikikusanya
maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi ili kupata sera
iliyoridhiwa na wengi.
Katika
sekta ya Ardhi Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Taifa
ya Ardhi ya 1995 kwa takribani miaka 20 hadi sasa, hata hivyo
zimejitokeza changamoto nyingi ambazo zinalazimu kufanya mapitio ya sera
hiyo.
Migogoro
na malalamiko yanayotokana na ardhi ni changamoto zinazo chukua nafasi
kubwa katika jamii yetu na imekuwa ikiigharimu kwa kiasi kikubwa katika
kuitatua.
Hamisi
Maduka Kaimu mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani
Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha
Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alisistiza ulipaji wa fidia za
Ardhi uzingatie uhalisia wa thamani ya eneo husika.
Kuongezeka
kwa migogoro hii imekuwa ni changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi
pamoja na watumiaji mbalimbali wa ardhi hususan wakulima na wafugaji,
wawekezaji, wananchi, vijiji na hifadhi.
Hata
hivyo, kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji hususan
katika sekta za kilimo, madini, viwanda na wananchi kutonufaika na
uwekezaji unaofanywa katika ardhi na hivyo kusababisha migogoro baina ya
wananchi na wawekezaji.
Aidha
kutokuwepo kwa mipango ya matumizi endelevu ya ardhi mijini na vijijini
na hata sekta ya ardhi kuvamiwa na madalali ni changamoto iliyoifanya
Serikali kuamua kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995.
Changamoto
zote kwa pamoja, zimelazimika kufanyika kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya
Ardhi ya 1995 ili kutoa mwelekeo mpya na usimamizi wa ardhi kwa manufaa
ya watanzania wote.
Abdallah
Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa
maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya
Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki
kwa wanavijiji.
Ardhi
ni Sekta mama na hivyo basi Sera ya ardhi ni sera mama katika masuala
yote ya maendeleo ikiwemo kilimo na mifugo, ambayo shughuli zake
zinafanyika kwenye ardhi.
Na
sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la
ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili
kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha
kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya
Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi,
Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.
Shakira
Masudi mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa
maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya
Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa
maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.
Mwl.
Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo
mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi
ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena