Mchezaji
wa klabu ya Dinammo Bucharest ya Romania raia wa Cameroon, Patrick
Ekeng, 26 ameanguka uwanjani na kupoteza maisha wakati timu yake
ikicheza mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Viitorul Constanta.
Katika
mchezo huo uliomalizika kwa sare ya goli 3-3, Ekeng alianguka dk. 69
ambapo mchezo ulisimama kwa dakika saba ili kupisha wahudumu wa afya
kuona ni jinsi gani wataweza kuokoa maisha yake lakini ilishindikana.
Hali
ya huzuni ilitawala zaidi baada ya Msemaji wa Hospitali ya Floreasca,
Cristian Pandrea kutoa taarifa za kifo cha Ekeng na kueleza kuwa
madaktari walijitahidi kuokoa maisha ya Ekeng bila mafanikio.
Patrick Ekeng akiwa chini baada ya kuanguka wakati mchezo ukiendelea.
Mchezaji
huyo wa Cameroon alikuwa akiishi Romania na mke wake pamoja na motto
wake wakiishi Paris, Ufaransa na kuna taarifa kuwa alikuwa aende
Ufaransa kuungana na familia yake siku ya Jumanne baada ya fainali ya
Ngao ya Hisani nchini humo. Mke wake anatarji kuwasili Romania leo
Jumamosi.
Ekeng
anakuwa siyo mchezaji wa kwanza wa Dinammo Bucharest kwani hata Octoba,
2000 aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Catalin Hildan alianguka na
kupoteza maisha.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena