Imeadndaliwa na
Catherine Masiko
Jambo Rafiki!
Karibu tukumbushane!
TOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME!
wanawake na wanaume wako na tofauti kubwa katika vitu zifuatazo!
MITAZAMO, MISONGO, KUPENDA, MOTISHA , LUGHA, URAFIKI/UKARIBU, na katika MIJADALA AU UBISHANI
Tofauti katika MITAZAMO
Katika mitazamo wanaume wanatoa majibu ya moja kwa moja kwa wake zao ama wenzi wao ( ndio ni ndio hapana ni hapana hatoi maelezo) ila mwanamke hutoa ushauri tena kwa maelezo
Lakin mwanaume wakitoa majawabu ya moja kwa moja mwanamke hujickia vibaya huona kama ana onewa lakin iyo ni tabia ya mwanaume ndivyo aliumbwa (anajibu kama alivyoulizwa hatoi Maelezo)
Mwanaume hapendi kuambiwa nini cha kufanya anapenda afanye au aweke wazo then mwanamke amshauri
Tofauti katika MISONGO
Mwanaume akiwa na misongo hupenda kua mbali mahali patulivu pekee yake au akiwa na misongo huku akiwa nybani hapendi kuulizwa maswali ama kuogeleshwa
Ila mwanamke akiwa na misongo hupenda kuongea sana bila kunyamaza husema saaana kuhusu jambo lililopo moyoni mwake linalo msumbua yani nitfauti na wanaume huwa kimya pekee yao ila mwanamke hupenda kuongea saana yote yaishe moyon mwake mwanaume ukiona mke yuko ivyo muache aongee yoooooote amalize mana ndivyo alivyo umbwa na hiyo ndio dawa yake
Usianze kusema mbona unaongea sana ukaanza kumkaripia ukiona ivyo ujue ako na Shida moyoni kwake!
Tofauti katika KUPENDA
Kwanza mwanaume na mwanamke hutoa aina ya upendo amabao wanataka waupate sio abao wenzi wao wanautaka
Mwanaume hupenda kwa kutazama/kuona kusikia na kuhisi, wanaume wanataka kuaminiwa for sure uwaamin uwakubali na watambuliwe kwa huduma yao
Mwanamke hupenda kwa kushika kuhakiki kitu, mwanamke hukinai/huridhika mapema akijaliwa kuheshimiwa kueleweka kuthaminiwa hata wakati mwingine mkitembea wamshika mkono anajickia anapendwa
Means mwanamke anapenda kwa kuonyeshwa upendo!(kuhakikishiwa)
Tofauti katk MOTISHA
Wanaume hupata motisha/ari wanapojickia wanahitajika au ni wa mhima
Chukulia mfano TV imeharibika pale nyumbani Mme amejitahid kutegeza akashindwa mke hupaswi mwambia NILJUA TU HUWEZI KUTENGENEZA no mwache mwenyewe tena wee nenda jikoni kabisa ukapike akishidwa kutengeza atatafuta fundi atatengeeza then mpongezee kwa jitihada alizofanya, apo anajickia ni wa mhimu anahitajika
Mwanamke hupata motisha anapoajickia anapendwa! Anathaminiwa
Tofauti katika LUGHA!
Wanaume hueleza ama huelewa vitu moja kwa moja sio kwa maelezo ukitoa maelezezo unamchanganya akili ya mwanaume ni tofauti na ya mwanamke, ndio maana mwanamke anaeza kufanya vitu viwil kwa wakati mmoja (anaeza kua anaonge na wewe huku anachapa kwa computer kitu ambacho mwanaume hawezi kufanya)
Mfano: mwanamke, mwambie mmeo naomba shiling elf 50000 kwajili ya nguo! Usinze unajua ile nguo uliyoninunulia imeachoka lakini naipenda nilkua natamaan kununua nyingine ya aina ile ......na akikupa usiingize tena habari ya kununua viatu, njia rahisi ni hii wewe piga hesabu unahitaji nini na nini then peleka yote kwa pamoja usipeleke kila kitu kwa wakati wake....mmmmh hapo unamchnaganya mwanaume kwakwel
Katik lugha mwanamke hueleza kwa msukumo wa hisia akiwa anahitaji kitu Fulani wao awaji direct kama mwanaume no wao huzunguka saaaaana mpaka baadae wanafikia kwenye point ya msingi lakini akiwa amezunguka sana
Tena wakati mwingine wanazia mbali tangu mezan kwa chakula hehehe
Utamsikia dear umekipenda chakula? Umeshiba? Okay lakin honey unajua nilkua naomba .......ndo anaingiza sasa shida yake......so wanaaza mbali sana mpaka kufikia point yao ya msingi ( wakati mwingine utaitwa majina Mazuri Mazuri honey, Darling n.k na wakati huo hata sauti yake hubadilisha pia, ndivyo tulivyo
Tofauti katika URAFIKI!
Wanaune huwa karibu na wake zao but sometimes wanakua mbali ili waweze kuwa karibu tena ( wakati mwanaume anapokua mbali na mke wake mwanamke huogopa sana huenda amemkosea)
Na unapozidi kumuuliza vip kuna nn mbona uko hivyo anakumbia am okay niko sawa mke wangu mke niambie if nimekukosea baba no hujankosea sometimes wanaamua kuomba msamaha bila kujua kosa sivyo mwanamke ukiona mme wako ako hivyo take it easy tu ujue ndio wakati yuko mbali ili atafute vitu vya kukufurahisha wewe zaidi na hiyo hali huja automatically
Wanawake ni kama raba bend unatakiwa kumvuta ili awe karibu na wewe, vile unamvuta kwa upendo ndivyo anakua karibu na weee zaid kama raba bend once ukivuta ukiivuta zaid na zaid ndivyo yazid kuvutika kuja kwako so ni sawa na wanawake na unamvuta kwa vitu vidogo vidogo tu si lazima mambo makubwa ( vitu kama Muda) hakuna kitu mwanamke anahitaji zaid kuliko muda wako walkua nae, kumwangalia!
Wanawake ni kama wimbi la bahari vile linapanda na kushuka wimbi upepo ukivuma nalo huamka na upepo ukitulia nalo hutulia
Hivyo hivyo na wanawake ni kama wimbi la bahari akiwa maetulia hutoa upendo na ukaribu sana
Na kuna wakati unafika mwanmke anakua na furaha automatically na kuna wakati anakua mkimya tu automatically kama wanaume wanapokua kimya wakati wa msongo
So ukimuona mke wako ako na furaha siku hivyo anacheka tu usiaze kumkaripia MBONA UNACHEKA CHEKA OVYO?? no nenda naye ivyo ivyo utashangaa ancheka mpaka anakuletea mkono mgonge nawewe peleka mgogeshe na utaiona furaha na tabasam halisi
Wanawake wanapoona wanajali wenyewe awajaliwi ni wepesi sana kukata tamaa means wanapoona awarudishiw vile wametoa apo ndipo wimbi hupanda sana na kugongagonga
Wakati huo Mme watakiwa kuchukuliana nae ktk hali iyo na kumuonesha upendo na kumrudisha kwa hali yake ya kawaida
Tofauti katka MIJADALA
Wanaune kwa asili hutenda kama waliosahih siku zote wanaume siku zote hujiona awakosei ndio maamna uwa ni watu wa amri na sio rahisi kujishusha
Wanawake kwa kutokujua mwanaume kama iyo ni asili yake (amri) (kutokujishush) hudharau hiyo hali na kuanza kujihami na kuishi kwa woga sana!
*****""*************************************"****
Bwana abariki family zilizoko na zile zijazo!
*****""*************************************"****
Bwana abariki family zilizoko na zile zijazo!
Amen!
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena