Na Otaigo Elisha & Thomas Nkaina Utegi Habari watanzania Kilimo cha mchicha ni Kilimo ambacho ni kilahisi sana na kwa MTU wa kawaida na mwenye eneo dogo na mtaji mdogo anaweza kukifanya na kikamkuzia mtaji na kumsaidia katika kufanya Kilimo kingine chenye tija zaidi Kilimo chamchicha, kinahitaji eneo lilio na rutuba ya kutosha. Hivyo ni vyema kutumia Mbolea ya kuku au mbuzi kama inapatikana, baada ya hapo unaandaa udongo wako vizuri unaurainisha vizuri maana mbegu za mchicha ni ndogo ndogo sanazinahitaji udongo tifutifu ili ziweze kuota vizuri, Mbegu, kuna aina kama tatu za mbegu ya mchicha japo aina moja iitwwayo LISHE unaonekana kufanya vizuri na kupendwa na wateja wengi Muda wa ukuaji na kuvuna Mchicha hutumia siku 21 mpaka kuvuna hivyo hata kama una eneo dogo na mtaji Mdogo unaweza kufanya Kilimo hichi ili kuwahakikishia wateja wako mboga kila wakati basi ni vyema unagawa shamba lako, katika makundi manne inamaana kila wiki utapanda mchicha na kila wiki utavuna, mchicha Kilimo hichi sio kwa wale tu wanaofanya biashara hata wale ambao hawafanyi biashara wanaweza kulima kwa jili ya matumizi ya nyumbani Madawa Katika Kilimo hichi utumiaji wa madawa ni Mdogo sana na kama uko. Sehemu nzuri basi hata dawa huwezi kutumia, hivyo ni nzuri kwa afya ya mtumiaji, Kama. Unaswali kuhusu Kilimo hichi usisite kuuliza kupitia namba: 0713594688 0784665683
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena