Header Ads Widget

Responsive Advertisement

News | Rwanda yafurahia kuhukumiwa kwa mameya

Rwanda
Rwanda imekaribisha uamuzi wa kuwahukumu washukiwa wa mauaji ya kimbari nchini Ufaransa lakini Rwanda inaona kuwa hatua hiyo haitoshi na ilichelewa sana ikiwa imekuja miaka 22 baada ya mauaji ya kimbari .
Mahakama ya Ufaransa iliwahukumu Octavian Ngenzi na Tito Barahira ambao ni mameya wa zamani wa Rwanda kifungo cha maisha jela baada ya kuwakuta na hatia ya mauaji hayo.
Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya Rwanda Faustin Nkusi ameiambia BBC kwamba nchini Ufaransa kuna kesi nyingi za washukiwa wa mauaji ya kimbari ambazo bado zinahitaji kufanyiwa kazi.
Amesema nchi ya Ufaransa inahifadhi washukiwa wengi sana wa mauaji ya kimbari kuliko nchi nyingine barani ulaya.
“Kuna washukiwa wengi tuliokwisha tuma nyaraka za kuwakamata, wakiwemo hata vigogo wa serikali ya zamani.kuna wengine ambao wanafwatiliwa na mashirika ya kupigania haki za manusura wa mauaji ya kimbari nchini humo.ni idadi kubwa ya washukiwa walioko Ufaransa,” ameambia BBC.
Image copyright
Mahakama ya Ufaransa iliwapa kifungo cha maisha jela, Octavian Ngenzi, 58 na Tito Barahira, 64 kwa kuwakuta na hatia ya mauaji yaliyotokea katika kanisa la Kabarondo mashariki mwa Rwanda.
Katika kanisa hilo watutsi wapatao 2000.
Wote waliongoza wilaya hiyo kwa kufwatana kwanzia mwaka 77 hadi 94 na mahakama ilisema walikuwa na uwezo, mamlaka na ushawishi mkubwa wa kuweza kusimamisha mauaji hayo.
Wamekanusha mashitaka dhidi yao wakisema wanasikitishwa na yaliyotokea nchini Rwanda.
Wana fursa ya kukata rufaa katika mahakama kuu ya Ufaransa.

Post a Comment

0 Comments