Ni uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta ya burudani hapa Tanzania. Ndani ya himaya hii, kunapatikana studio za gharama kubwa zilizosheheni mitambo ya kisasa. Kuna studio mbili za sauti huku idara hiyo ikiongozwa na mjuzi na msomi wa ukandarasi sauti na mtayarishaji muziki, Sarthak Tale kutoka nchini India.
Wanene Entertainment imezindua studio kubwa za kisasa ambazo kwa mujibu wao ni za kwanza Afrika Mashariki na Kati.
Uzinduzi wa studio hizi ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya burudani huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
Uzinduzi wa studio hizi ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya burudani huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mheshimiwa Wambura alisema studio hiyo itakuwa mkombozi kwa wasanii wengi ambao walikuwa wakipeleka kazi zao nje ya nchi kufanyiwa mastering. Pia amedai kuwa uwepo wa studio hiyo utawasaidia wasanii kuwa na kazi zenye ubora wa kimataifa.
Kwa hakika studio za Wanene zitakuwa mkombozi kwa tasnia ya burudani ya Tanzania na kuupa muziki wake hadhi ya kimataifa ambayo wasanii wamekuwa wakiitafuta kwa miaka mingi.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena