RORYA
Mkuu wa wilaya ya rorya ndugu Saimoni Kemori Chacha amewataka wananchi wa Rorya kutumia fursa zilizopo kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kuondokana na maisha tegemezi aliyasema hayo alipo tembelea kikundi cha Rorya jamii foundation kuangalia shuguli zao za uzalishaji za kilimo bora cha mboga na matunda kilichopo mji mdogo wa utegi ndugu chacha alikipongeza kikundi hicho kwa kazi nzuri wanayo ifanya kwani kikundi hiki kinautumia vizuri mto mori ambao unatiririsha maji msimu wote wa kiangazi.amewataka wana nchi wa rorya kuiga mfano mzuri wa kikundi hiki kutumia fursa hizi kwani rorya bila njaa inawezekana endapo wananchi watatumia mito kama mto mori ,mto mirare na ziwa vikitorya kulima mazao kwa njia za umwagilia watafanikiwa kujikomboa kiuchumi na kupata chakula na kuepukana na baa la njaa . Akiongea na kituo cha habari na mawasiliano cha utegi telecomcenta ndugu chacha amewataka wananchi wa Rorya kujikita kwenye shuguli za uzalishaji na kuachana na mambo ya maandamano yanayo andaliwa na vyama vya siasa
Like page ya Rorya Jamii Foundation Hapa>>>>>>>>>>
Rorya Jamii Foundation
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena