Umewahi kufikiria ama kujiuliza faida zinazopatikana kwa kumkumbatia mkeo ama mpenzi wako mkiwa mmelala? Rorya Finest Mediainakufunulia Katiba Uwanja wa Mahaba ili upate kufahamu yale yanayokupa faraja ya penzi kutokana na kumbatio karibu twende sawa.
HUPUNGUZA SHINIKIZO LA KISAIKOLOJIA
Unapomkumbatia mkeo ama mpenzi wako mkiwa mmelala husaidia kuzalisha kichocheo (homoni) cha furaha kiitwacho ‘oxytocin’. Homoni hii hufanya kazi ya kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na hupunguza shinikizo la kisaikolojia. Hilo pia hupelekea kupunguza hatari ya kupatwa na maumivu ya kichwa na maradhi mengine.
USINGIZI MARIDHAWA
Wanandoa wanapokumbatiana husaidia kulala vizuri. Tafiti mpya zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza ‘cortisol’ na hivyo hupunguza shinikizo la kisaikolojia. Pindi ‘cortisol’ inapopungua mwilini, moja kwa moja usingizi huwa mzuri na mwanana.
Unapomkumbatia mwandani wako huleta raha, hasa mambo yanapofikia kwenye hatua ya kucheza, lakini kabla ya hapo furahia ladha ya mgusano wa ngozi zenu kabla ya kusonga mbele… moyo wako unatakiwa kuuhudhurisha katika eneo na muda wa mgusano huo ili kujenga uaminifu na hisia za ushirika.
MAWASILIANO BILA MANENO
Kukumbatiana hutoa fursa kwa wapenzi ya kuwasiliana bila kuongea. Na hili ni jambo maridhawa kabisa kwa wanandoa kuzidi kuwa karibu.
NI DAWA YA FADHAA
Kimbilia kitandani ili kupata kumbatio la asali wako wa moyo; kumbuka kuwa kitanda kipo kwa ajili hiyo. Achana na kitabu, televisheni, simu, tablet na mambo mengine kama hayo. Kumbatio litakusaidia kumakinika na kupata utuvu.
HUWAPA HISIA ZA KURIDHIANA NA KUTOSHEKA
Mnapokumbatiana bila kuwa na lengo la kuingia kweye tendo la ndoa, mtapata hisia kubwa ya kuridhika na ndoa yenu. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa wanandoa wanaokumbatiana wanaridhika sana na ndoa zao kuliko wale wasiokumbatiana.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena