Header Ads Widget

Responsive Advertisement

News | Sitaki Ukuta Rorya, asema DC

Image result for maandamano ya chadema
RORYA
Mkuu wa wilaya ya rorya ndugu SAIMON KEMORI CHACHA amewataka wananchi wa wilaya ya rorya kuheshi tamko la serikali la kutokushiriki maandamano yanayo itwa UKUTA yanayo andaliwa tarehe 1/9/2016 na vyama vya siasa ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuvunja sheria ya kupigwa marufuku maandamano na serikali.amesema nikosa kushiriki maandamano itakuwa ni kupingana na serikali ambayo imepika marufuku maandamano nchi nzima .amesema siku hiyo wananchi wa rorya kwakuwa niwatu wanao penda amani umoja kila mtu nikuendelea kufanya shugili za uzalishaji mali na kujiongezea kipato kwa ajili ya maendeleo yao .ndugu chacha akiongea na kituo cha habari na mawasiliana cha utegi telecomcentre amesema halitakuwa jambo jema kwa wananchi wake wa RORYA kujiingiza kwenye matatizo ya kushindana na tamko la serikali la kupiga marufuku maandamano hayo ambayo hayana faida yoyote kwao bali ni kwa watu wachache kujitafutia umaarufu wa mda mfupi ambao nisawa na nguvu ya soda. amesema yeye kama mkuu wa wilaya ya rorya hayuko tayari kupokea malalamiko ya watakao shiriki maandamano hayo. bali yuko tayari kwa kusikiliza shida na changamoto zinazo wakabili wananchi kwa ajili ya maendeleo yao na si vinginevyo

Post a Comment

0 Comments