Header Ads Widget

Responsive Advertisement

News | "Wataalam Nendeni Vijijini mfanye kazi", Asema DC Rorya


Na Thomas Nkaina
RORYA 
Mkuu wa wilaya ya rorya ndugu Saimon Kemori Chacha amewataka viongozi wa halimashauri ya wilaya ya rorya kwenda kwa wananchi na kufanya vikao na kuelezea mipango ya serikali pindi serikali inapo toa pesa za miradi ya maendeleo wahakikishe taarifa zina wafikia wananchi ili wafahamu mipango ya serikali yao. Chacha ameyasema haya wakati akifunga baraza la madiwani la halimashauri ya rorya. Kuhusu suala la halimashauri kuto kuwa na mwanasheria mwenye elimu ya uwanasheria ya kutosha itapelekea halimashauri kuendelea kuwa na migogoro hasa ambayo ndio kero kubwa kwa wananchi kuhusu mambo ya kisheria ya ardhi .Amewataka mwenyekiti wa halimashauri na mkurugenzi kufuatilia serikalini na kupata mwana sheria mapema iwezekanavyo. nae mwenyekiti wa halimashauri Mh Machiwa amesema kuna haja ya kufanya marekebisho kwenye minada ya Randa na Obwere Shirati ili kuwepo na nidhamu ya mapato kwani mapato yanayo kusanywa kwenye masoko hayo sio stahiki ya masoko hayo .

Post a Comment

0 Comments