Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TeknoWorld | Transit elevated Bus | Basi linalopita juu ya magari lajaribiwa huko China

Siku kadhaa zilizopita ziliripotiwa taarifa za kutengenezwa kwa basi la umeme lenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine huko China. Kutokana na China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Duniani, hivyo basi hilo linatajwa kuwa ufumbuzi sahihi wa msongamano wa magari barabarani, imeelezwa kuwa basi hilo tayari limevutia serikali za Brazil, Ufaransa , India na Indonesia.
36D14DC600000578-3606602-image-a-28_1470177582302
Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu hao kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao mwezi May, wiki hii basi hilo limefanyiwa majaribio kwenye eneo la kaskazini mwa China jimbo la Hebei katika barabara iliyofanyiwa ukarabati yenye urefu wa mita 300, basi hilo lina uwezo wa kuhudumu kwa kasi ya kilometa 60 kwa saa na litakuwa na uwezo wa kubeba watu 1200 kwa wakati mmoja.
36D14DCB00000578-3606602-image-m-26_1470177506057 36D14DD200000578-3606602-image-a-19_1470177460651 36D14DD600000578-3606602-image-a-27_1470177514106 36D14DDA00000578-3606602-image-a-32_1470177737069
Unaweza kuangalia video hii hapa chini

ULIKOSA HII YA DIAMOND KUTAJA NGOMA ZAKE 5 ZINAZOKUBALIKA KIMATAIFA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Post a Comment

0 Comments