Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NEWS | TIGO Wakamkabidhi DC Rorya Madawati 135


Na Thomas Nkaina
RORYA :


Mkuu wa wilaya ya RORYA ndugu SAIMONI KEMORI CHACHA ameipongeza kampuni ya simu ya TIGO kwa msaada mkubwa walioutoa wa madawati 135 kwa wilaya ya rorya amesema ushirikiano wa wilaya ya rorya na kampuni ya tigo ni mkubwa na kusema tigo ni wadau wa maendeleo. msaada huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza uhaba wa madawati na kufanya mpango wa serikali wa elimu bure kufanikiwa . akimkaribisha mkuu wa mkoa wa mara ndugu CHARLES MULIGWA ili aweze kupokea madawati kutoka kwenye kampuni ya TIGO amesema kampuni zingine zinapaswa kuiga mfano wa kampuni ya tigo kwa kuwekeza kwenye shuguli za kijamii hasa elimu. 

Mkuu wa mkoa wa mara ndugu CHARLES MULIGWA akizungumza na wananchi walio fika kushuhudia kampuni ya tigo ikitoa msaada wa madawati kwa wilaya ya rorya mkuu wa mkoa amesema anamshukur raisi magufuli kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa mara akasema kauli mbiu ya raisi ya HAPA KAZI TU naye pia ni hapa kazi tu pia kampuni ya tigo nayo imeungana na serikali ya hapa kazi tu. kwa kuunga mkono serikali kwa juhudi za elimu bure kwa kila mwanafunzi kukalia dawati na kwa rorya sasa tatizo la madawati limepungua kwa kiasi kikubwa .ameiomba kampuni ya tigo kwakuwa wao ni wadau basi ombi la mkurugenzi wa halimashauri ya rorya la kampuni ya tigo kusaidia mabati kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa anaimani tigo watasaidia ili kupunguza tatizo la madarasa. tukio hili la kukabidhi madawati katika wilaya ya rorya lilifanyikia shule ya msingi utegi




Post a Comment

0 Comments